Aliyekuwa rais wa Liberia
Charles Taylor ambaye amezuiliwa kwa makosa ya jinai, amewaandikia barua
wabunge wa nchi hiyo na kuwataka wamlipe malipo yake ya uzeeni dola
25,000.
Katibu wa baraza la senate, Nanborloh Singbeh amesema kuwa barua hiyo itaweza kujadiliwa na wabunge katika kikao cha wiki ijayo.Mwezi Mei mwaka jana, mahakama iliyokuwa inasikiliza kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Sierra Leone, ilimhukumu Taylor miaka 50 gerezani kwa makosa 11 ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Taylor ndiye rais wa kwanza wa zamani kufungwa jela na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita tangu kesi zilizowahusu waliokuwa watawala wa Nazi baada ya vita vya pili vya dunia.
Hata hivyo Taylor, amekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama maalum ya Sierra Leone iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
Iliamua kuwa Taylor, aliunga mkono waasi waliofanya uasi nchini Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991-2002.
Hata hivyo, imebainika kuwa barua hiyo ina makosa kadhaa ya kisarufi,
Kilio cha Taylor kimesababisha maswali kuhusu ikiwa Taylor ndiye aliandika barua hiyo.
Hata hivyo, shemeji yake Taylor Arthur Saye aliambia waandishi wa habari kuwa rais huyo wa zamani ndiye aliandika barua hiyo.
No comments:
Post a Comment