Raia wawili wa Misri wameuawa na
wengine wawili kujeruhiwa, kwenye shambulio liliotekelezwa dhidi ya
kanisa moja la Coptic mjini Misrata.
Afisa mmoja wa baraza la mji huo ameiambia BBC
kuwa kumetokea mlipuko ndani ya jengo la kanisa hilo wakati wanne hao
walipokuwa wakila chakula chao cha mchana.Haijulikani ni nani aliyefanya shambulio hilo mjin Dafiniyah, viungani wa Misrata.
Hata hivyo kuna habari za kutatanisha kuhusu ni lini shambulio hilo lilitokea.
Afisa huyo asema kanisa hilo lilishambuliwa kwa bomu la kujitengenezea, kwa kuwa baruti zinazotumika kwa uvuvi zilipatikana katika eneo hilo
Shirika la habari la serikali limesema kuwa, serikali ya nchi hiyo imeagiza maafisa zaidi wa polisi kutumwa katika kanisa hilo.
Serikali ya Misri imeagiza uchunguzi
Waziri wa mambo ya nje wa Misri, Mohammed Kamel Amr, amesema, serikali imeagiza uchunguzi kufuatia tukio hilo na kusema waliohusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.Kuna idadi ndogo sana ya wakristu nchini Libya, wengi wao wakiwa raia wa kigeni.
Baadhi yao wahamiaji kutoka Misri ambako waumini wa kanisa la Coptic ndilo dhehebu kubwa zaidi la Kikristo.
Serikali ya Libya imekuwa ikikabiliana na matatizo wa kuhakikisha usalama tangu kuondolewa madarakani wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka uliopita.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mashambulio ya kigaidi dhidi ya majengo ya kibalozi na yale ya mashirika ya kutoa misaada na mwezi Septemba mwaka huu, Ubalozi wa Marekani, mjini Benghazi ulishambuliwa na balozi wa Marekani na maafisa wengine waliuawa.
No comments:
Post a Comment