Wednesday, January 16, 2013

Okwi atua Etoile kwa dola 300,000



BAADA ya kuhangaika muda mrefu hatimaye mshambuliaji wa mabingwa wa Tanzania Bara, Simba na timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi amejiunga na

klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa gharama ya Ddola 300,000 (sawa na Sshs 477 milioni).

Okwi alisaini mkataba huo wa kuichezea timu hiyo kwa

muda miaka mitatu na nusu mbele ya Mmwenyekiti wa Simba,

Ismail Aden Rage na Rrais wa Etoile, Ridha Charfeddine

jana Jumanne mchana.

Okwi ambaye mwishoni mwa mwaka jana aliongeza mkataba

wa kuichezea Simba mpaka mwaka 2014, ameuzwa kwa D

dola za kimarekani 300,000, na kuweka rekodi ya mauzo ya

juu kwa klabu hiyo.

Katika mkataba huo Okwi aneweka kibindoni dola

100,000 kwa kukubali kusaini mkataba huo pamoja na

kulipwa mshahara wa Ddola 15,000 kwa mwezi.

Habari hiyo iliyothibitishwa na OAfisa Habari wa klabu hiyo,

Ezekiel Kamwaga zilisema kuwa Simba iliwakilishwa na

mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage kukamilisha

zoezi hilo.

Okwi aliyekuwa katika majaribio na timu hiyo uhamisho

wake ulifanyika harakaa haraka ili kuwahi mwisho wa usajili

wa nchi hiyo.

Mchezaji huyo wa Uganda, mara kadhaa amekuwa gumzo

katika usajili na katika dirisha dogo, liliwalazimu viongozi wa

Simba kumfuata Uganda na kumsainisha kwa miaka miwili.

Hatua hiyo ilitokana na uvumi kuwa mchezaji huyo alikuwa

na mpango wa kujiunga na watani wa jadi wa Simba, Yanga

na klabu ya Azam FC ambazo zilidaiwa kutoa ofa kubwa

kwa mchezaji huyo.

Katika usajili wa mwanzoni mwa mwaka jana, Okwi alikimbilia

kusaka timu nje ya nchi, hata hivyo pamoja na kufanya vizuri,

hakuweza kucheza huko na kurejea katika timu yake ya

Simba.
O
Afisa Habari wa klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga

alisema kuwa ni kweli kuwa Okwi ameuzwa kwa timu hiyo,

hata hivyo hakuwa tayari kuweka bayana masuala mbali

mbali ya mkataba wa mchezaji huyo.

“Nipo likizo, taarifa hizo ni za kweli, lakini kutokana na hali

ilivyo, mwenyekiti wa timu, Rage atakuja kuelezea kwa kina

suala la mchezaji huyo na kuhusiana na marlupurlupu mengine

pamoja na makubaliano hasa mshahara, kwa sasa sina

taarifa zaidi ya kuuzwa kwa mchezaji huyo,” alisema

Kamwaga.

Alisema kuwa anajua kuwa Okwi hakwenda na timu Oman

kwa ajili ya mazoezi ya maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu ya

Tanzania Bara na michuano ya kimataifa na vile vile anajua

taarifa za kuondoka kwa Rage kwenda huko kukamilisha

zoezi la mauzo ya mchezaji huyo.

Miaka miwili iliyopita, Simba iliuzwa wachezaji wake wawili,

Mbwana Samatta and Mganda Patrick Ochan kwa klabu

ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa Ddola

100,000 (Sshs150 milioni ) kila mmoja.

Kutokana na kuuzwa kwa Okwi, Simba sasa inabakiwa na

wachezaji wanne wa kigeni, Mzambia Felix Sunzu, Komabil

Keita (Mali), Mussa Mudde na kipa Abel Dhaira kutoka

Uganda.

No comments:

Post a Comment