Michael Laudrup amakiri kuwa
ushindi wa Swansea wa magoli mawili kwa bila dhidi ya Chelsea katika
raundi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la ligi, ulikuwa wa
kushangaza.
Makosa yaliyofanywa na mlinda lango wa Chelsea
Branislav Ivanovic ilisababisha Michu na Danny Graham kuifungia Swansea
magoli hayo katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Stampford Birdge.Raundi ya pili cha mechi hiyo itachezwa tarehe 23 mwezi huu katika uwanja wa nyumbani wa Swansea.
Chelsea ilithibiti mpira kwa asilimia kubwa lakini makosa hayo yaliyofanywa na Ivanovic yalisababisha matumaini ya Chelsea ya kufuzu kwa fainali za kombe hilo kudidimia.
Goli la Chelsea lakataliwa
Katika dakika za mwisho za mechi hiyo Ivanovic vile vile akafanya kosa lingine la kupeana pasi, bila kumtizama mlinda lango mwenzake, na kuumpa nafasi Graham ya kufunga bao la pili.
Goli lililofungwa na mshambulizi wa Chelsea Demba Ba dakika ya tisini ilikataliwa na msaidizi wa refa ambaye alisema kuwa, Ba alikuwa ameotea.
Laudrup aliwapongeza wachezaji wake kwa kutumia fursa walizopata wakati wa mechi hiyo.
Mshindi kati ya Chelsea na Swansea atacheza na mshindi kati ya Aston Villa na Bradford City.
No comments:
Post a Comment