Hata hivyo habari za uhakika zilizopatikana jana
na kuthibitishwa na polisi zilisema wengi wa waliobiwa kwa njia hiyo
hawatoi taarifa polisi japo matukio hayo yanaongezeka.
Watu wanaoendesha vitendo hivyo kwenye maegesho ya
magari wanadaiwa kumwaga kemikali kama mafuta ya nywele za wanawake
aina ya Curl ambayo hupasua kioo na kukiacha kama chengachenga.
Kikundi hicho kinadaiwa kulenga zaidi vifaa vya
thamani kama kompyuta mpakato(Laptop),Kamera, fedha taslimu, simu za
mikononi na pochi za wanawake ambazo kwa sehemu kubwa huwa na vito vya
thamani na fedha.
Mthamini wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Hugo
Michael ni mmoja wa waathirika wa tukio hilo ambaye alisema, binafsi
aliibiwa mfuko uliokuwa na Laptop, Kamera na nyaraka mbalimbali za
ofisi.
Alisema Jumatatu iliyopita aliegesha gari eneo la
maegesho ya hospitali ya Rufaa ya KCMC na kwenda kumuona mgonjwa lakini
aliporejea alikuta kioo cha gari yake kimepakwa mafuta na kusambaratika.
Mhandisi wa mradi mkubwa wa jengo la kibiashara la
mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) karibu na Halmashauri naye alikumbwa
na tukio kama hilo na kuibiwa Laptop na nyaraka mbalimbali.
Mbali na wizi huo ,eneo la Soko la Mbuyuni, nako
kumeibuka wimbi la wizi wa vitu mbalimbali kwenye magari yanayoegeshwa
eneo hilo ambapo wezi hao hufungua milango na vioo vya magari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
alisema matukio ya wizi wa kutumia kemikali bado hayajamfikia lakini ya
wizi katika soko la Mbuyuni wana taarifa nayo na wanaendelea na
uchunguzi.
Alisema polisi wamefanikiwa kukamata watuhumiwa
wachache wanaodaiwa kuhusika na wizi huo lakini wanashindwa kuwafikisha
mahakamani kwa kukosa ushirikiano kutoka kwa wanaoibiwa.
CHANZO -MWANANCHI
CHANZO -MWANANCHI
No comments:
Post a Comment