Lakini sasa sivyo ilivyo.
Uchaguzi unafanywa katika hali tulivu na ya kidemokrasi.
Uchumi unakuwa kwa haraka ingawa ulikuwa umeanguka sana wakati wa vita.
Na bado Sierra Leone ni nchi maskini.
Rais Ernest bai Koroma anapingwa na wengine kadha katika kuania urais.
Uchaguzi unasimamiwa na maelfu ya wachunguzi wa Sierra Leone wanaolipiwa na serikali ya Uingereza.
Jeshi la Uingereza lilingilia kati nchini Sierra Leone mwaka wa 2000 kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa hivo ni sawa kwa serikali ya Uingereza sasa kugharimia usimamizi wa uchaguzi ili kuhakikisha kuwa serikali mpya imechaguliwa kwa njia za kidemokrasi na halali.
chanzo-bbc.com
No comments:
Post a Comment