Muimbaji
mahiri wa kike hapa nchini Judith Wambura (kulia) almaarufu kwa jina la
Lady Jay Dee akizungumza na waandishi wa habari leo katika mgahawa wake
wa ‘Nyumbani Lounge’ uliopo jijini Dar es Salaam na kutambulisha rasmi
kipindi chake kipya cha luninga kitakachoitwa‘Diary ya Lady Jay Dee’.
Amesema
madhumuni ya kipindi hicho ni kuleta burudani tofauti kwa wapenzi wa
muziki wake na muziki wa kizazi kipya kwa ujumla, vilevile kitatoa
fundisho na changamoto kwa wasanii chipukizi kujua wasanii wakongwe
wamepitia katika vikwazo gani.
Lady Jay Dee amesema kipindi
hicho kitaonyeshwa ndani ya East Africa Television kuanzia tarehe 18
Novemba mwaka huu kila siku ya Jumapili.
Aidha ametumia fursa
hiyo kutoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kushiriki katika
kudhamini vipindi vinavyobuniwa kama hivyo ili kuweza kutoa ajira kwa
wasanii na wadau wengine wa sekta ya muziki na burudani.Kushoto ni Mkuu
wa Vipindi wa East Africa TV Bi. Lydia Igarabuza
Mkuu
wa Vipindi wa East Africa TV Bi. Lydia Igarabuza akizungumzia jinsi
stesheni hiyo ilivyopokea kwa shangwe kipindi hicho na kuwa kitakuwa
hewani Jumapili saa 3 usiku kuanzia Novemba 18 na kuwataka vijana wa
Afrika Mashariki kukitazama ili kujifunza mengi kutoka kwa watu ambao
tayari wanamafanikio kupitia tasnia ya muziki.
No comments:
Post a Comment