Kocha wa livepool Brendan
Rodgers amesema nyota wake Luis Suarez atasalia na klabu hiyo na
kukariri kuwa hakuna klbau yoyote ambayo imeonyesha nia ya kumsajili
mchezaji huyo.
Klabu ya manchester City imeripotiwa kuonyesha
nia ya kumsajili Suarez, 25,. Mapema msimu huu mchezaji huyo kutoka
Uruguay alisaini mkataba mpya na klabu hiyo na amekuwa katika hali nzuri
ambapo amefunga jumla ya magoli 11 baada ya kucheza mechi kumi na sita.'' Ikiwa tutampoteza Luis, basi hatutakuwa na washambulizi, na kwa sasa sina uwezo wa kumpoteza yeyote'' alisema Roggers.
Suarez alilipwa kitita cha puani milioni 22.7 wakati alipokihama klabu ya Ajax na kujiunga na klabvu ya Liverpool Januari mwaka wa 2011.
Katika msimu wake wa kwanza na Liverpool, Suarez alifunga magoli 17 baada ya kucheza mechi 39.
Hata hivyo mchezaji huyo amekumba na mizozo kadhaa akiwa England.
Suarez alipatikana na hatia ya kutumia lugha ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mlinda lango wa Manchester United Patric Evra, na kupigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi nane.
Vile vile alishutumiwa kwa kutomsalimia Evra wakati wa mechi yao katika uwanja wa Old Trafford.
No comments:
Post a Comment