VIONGOZI HAO WALIFIKISHWA HAPO SAA TATU ASUBUHI AMBAPO KABLA YA HAPO
MAKACHERO WA ASKARI POLISI WALIWAHI KUFIKA ILI KUWEZA KUWAZUIA WANANCHI
WASISOGEE KATIKA ENEO HILO IKIWA NI AGIZO MAALUM KUTOKA KWA VYOMBO VYA
ULINZI KUTOKANA NA KITENDO KISICHOTARAJIWA ALICHOKIFANYA SHEHE FARIDI
CHA KUWAULIZA WANANCHI KUHUSU MUUNGANO NA WAO KUJIBU KWA SAUTI MOJA
KWAMBA HAWAUTAKI WAKATI WALIPOKUA WAKITOKA KATIKA KESI ILIOENDESHWA
TAREHE 20-11-2012 MAHAKAMANI HAPO VUGA.
MADAI HAYO
YALIWASILISHWA KWA DPP RAYA MSELEM NA RAMADHAN NASIBU CHINI YA JAJI
MKUSA ISAC SEPETU. AMBAPO DPP HAO WAMEOMBA WAPATIWE SIKU KUMI NA NNE
KUWEZA KUIPITIA SAMAS YA KESI HIYO KWA KUWA HAWAKUTAARIFIWA MAPEMA.
NA KWA UPANDE WA MAWAKILI WA WASHTAKIWA HAO ABDALLAH JUMA NA SALUM
TAWFIQ WAMESEMA HAWAPINGANI NA MAOMBI YA DPP HAO KWA KUWA WANAHAKI YA
KISHERIA KUDAI MUDA LAKINI WAMESEMA MUDA WALIOTOWA NI MKUBWA HIVYO
WAMEIOMBA MAHAKAMA WAUPUNGUZE MUDA ILI KUWEZA KUJUA KAMA KUNA ULAZIMA
WA KUONGEZA MADAI MENGINE AU HAYO WALIOYATOWA YANATOSHA.
AIDHA
WAMEIOMBA MAHAKAMA KULITILIA MKAZO SUALA KUPUNGUZIWA MUDA KWA KUWA
BADO WATEJA WAO WAPO RUMANDE HIVYO KADRI WANAVYOENDELEA KUKAA NDIVO
UONEVU UNAVYONGEZEKA.
BAADA YA MVUTANO MKUBWA KATI YA UPANDE WA
DPP NA MAWAKILI HAO JAJI ISAC SEPETU AMESEMA SHERIA YA GEREZA NO 2 YA
MWAKA 2007 ITEKELEZWE, NA BAADAE KUAMUA KUWAPA WIKI MOJA KUWEZA
KUYAPITIA NA BAADAE KURUDI TAREHE 29-11-2012 KWA AJILI YA KUSIKILIZWA
NA KUTOLEWA UFAFANUZI WA MADAI HAYO…
No comments:
Post a Comment