West Ham imetangaza kuwa itao
adhabu kali kwa mashabiki wake ambao watapatikana na hatia kutumia lugha
ya ubaguzi wa rangi wakati wa mechi yao siku ya Jumapili, dhidi ya
Tottenham.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa klabu hiyo
mashabiki watakaopatikana na hatia huenda wakapigwa marufuku ya
kutohudhuira mechi yoyote ya klabu hiyo maishani.Shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza, FA limesema linachunguza uwezekano wa kuanzisha uchunguzi kufuatia ripoti kuwa mashabiki kadhaa wa Tottenham walidhulumiwa.
Inadaiwa kuwa baadhi ya mashabiki wa Westham, waliimba nyimbo za ubaguzi kuhusiana na kujeruhiwa kwa mashabiki wa Tottenham mjini Rome wiki iliyopita ambako baadhi yao walidungwa visu.
Tayari malalamisha kadhaa yamewasilisha kwa idara ya polisi na klabu hiyo imetangaza kuwa itachukua hatua kali zaidi dhidi ya mashabiki watakaopatikana na hatia.
Msemaji wa FA, amesema wanasubiri ripoti ya maafisa waliosimamia mechi hiyo, ili kuamua hatua watakayochukua.
Baadhi ya mashabiki wa Westham, wanadaiwa kuwakejeli mashabiki wa Tottenham, ambao tangu jadi wamekuwa na uhusiano wa karibu na jamii ya Wayahudi wanaoishi mjini London.
No comments:
Post a Comment