MMOJA wa
watu waliokaribu sana na marehemu Sharo Milionea, Mzee Majuto jana
alizirai msibani wakati mwili wa marehemu ukiwa njiani kuletwa nyumbani
kutoka hospitali tayari kwa mazishi.
Majuto
ambaye kwa wakati fulani alionekana kujitahidi kuwa imara, alijikuta
akichotwa na hisia kali na kudondoka chini na kisha kupoteza fahamu kwa
dakika kadhaa.
Hatimaye
baada ya juhudi ningi za kumpepea, Mzee Majuto alizinduka na
kupumzishwa kando ili aweze kurejea katika hali ya kawaida.
Akiongea
na Saluti5 baadae, Mzee Majuto alisema kifo cha Sharo kimemuumiza sana
“Nahisi kama nusu ya mwili wangu umechukuliwa, ni mtoto mdogo lakini
alikuwa rafiki yangu sana, alikuwa zaidi ya mwanangu” alisema kwa
uchungu mzee Majuto.
Kwa
miaka ya hivi karibuni Mzee Majuto na Sharo Milionea wamekuwa ndio
wasanii wanao-oana zaidi kikazi kiasi cha kupelekea makampuni kadhaa
kuwatumia kwenye matangazo yao ya biashara.
No comments:
Post a Comment