ZIARA za nje za Rais jana ziligeuka hoja kuu wakati wajumbe wa tume ya
maoni ya Katiba walipokutana na wananchi wilayani Karatu ambapo baadhi
walipendekeza Katiba mpya ipange idadi ya ziara za Mkuu huyo wa nchi ili
kuwabana wenye hulka ya safari zisizo na tija kwa gharama na kodi ya
umma.
Phillipo Josephat (40), mkazi wa Rhotia wilayani Karatu
aliomba licha ya kupanga idadi maalumu ya ziara za nje ya nchi kwa Rais,
pia idadi ya watu anaoambatana nao idhibitiwe kupunguza gharama.
Utakuta
Marais wa nchi maskini kama yetu wanafanya ziara nyingi za nje wakiwa
na misafara mikubwa kuliko hata wenzao wa nchi zilizoendelea. Na kwa
sababu hawabanwi, kila anayeingia madarakani huamua kusafiri atakavyo
bila kuangalia faida na hasara za safari zake kwa Taifa,î alisema
Josephat.
Arther Gurti yeye alipendekeza Katiba iondoe mamlaka ya
uteuzi wa Jaji Mkuu na wajumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi mikononi
mwa Rais, badala yake nafasi hizo ziombwe kwa sifa za kitaaluma na
uadilifu wa
waombaji.
Alisema baada ya kuomba na kuchujwa,
majina machache yawasilishwe mbele ya kamati maalumu itakayoundwa na
bunge ambayo itawahoji na kupendekeza majina machache yatakayowasilishwa
kwa Rais kwa uteuzi wa mwisho kabla ya bunge zima kuidhinisha jina la
mteule.
Kwa upande wake, Orbano Michael yeye alitaka katiba mpya
imnyangíanye madaraka Rais kuteua watu 10 kuingia bungeni badala yake
aruhusiwe kuteua watu kushika madaraka ya Uwaziri kutoka nje ya bunge
ili kupanua wigo wa uteuzi unaotumika kuteua wabunge.
No comments:
Post a Comment