Tuesday, November 20, 2012

HUYU NDIO MSANII MWINGINE WA AFRICA ALIEREKODI NA KICHWA KUTOKA KWA RICK ROSS.


Millard Ayo na D Black
Staa wa hiphop kutoka nchini Ghana D Black ambae ni mshindi wa tuzo ya Channel O 2012 (Most gifted African west video of the year – falling) ameithibitishia AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kwenye exclusive interview kwamba ameingia kwenye list ya mastaa wa Afrika waliofanya kolabo na wasanii wakubwa wa dunia.
Baada ya kuwasikia wakali kama P Square na Rick Ross, D Banj na Good Music, STL na Mohombi, Ay na Romeo pamoja na Lamya na wengine, D Black amesema ameongezeka kwenye hiyo list baada ya kufanya kolabo na rapper Wale wa Maybach music.
D kasema hiyo kolabo alionganishiwa na BET wakati alipokwenda kuhudhuria tuzo zao ambapo alikutana na mastaa kibao na kufanya kolabo na kichwa kingine cha Cash Money ambacho sio maarufu sana.
Wale.
Anasema haikua rahisi na wala hakuna urahisi wa wasanii wa Marekani kukubali kolabo la nafasi yake ya kuwa nominated kwenye tuzo za BET ndio kumetoa nguvu ya huo muunganiko.
Album yake mpya ina kolabo zaidi ya 10 zikiwemo za Fally Ipupa, Ice Prince na wengine.
chanzo-millard ayo.com

No comments:

Post a Comment