PENYE
wengi hapokosi mengi, katika mazishi ya msanii nyota, Sharo Milionea
yaliyofanyika jana Lusanga, Muheza, zilipenya mbegu mbaya za imani za
kishirikina.
Msanii
mmoja mkongwe ambaye Saluti5 haioni busara kulitaja jina lake,
alithubutu kusema Sharo Milionea hakufariki bali amechukuliwa kama
msukule.
“Sina
la kufanya kwa kuwa mimi si mwanafamilia lakini ndani ya nafsi yangu
naamini Sharo hakufa, yupo hai amechukuliwa msukule” alisema msanii
huyo.
Sharo Milionea alifariki Jumatatu usiku kwa ajali mbaya ya gari wakati akielekea kwao Lusanga kumsalimia mama yake mzazi.
chanzo- Saluti5
No comments:
Post a Comment