MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kuanza kusikiliza
ushahidi wa walalamikaji katika kesi ya ubadhirifu inayomkabili Askofu
Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBC), Zakaria Kakobe
Aprili 2, mwakani.
Pia, mahakama hiyo imetoa siku 14 kwa pande zote
kukubaliana na kuwasilisha mahakamani hoja au mambo yanayobishaniwa,
ambayo ndiyo yatakayotolewa ushahidi.
Amri hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na
Jaji Iman Abood, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo wakati wa mkutano wa
makubaliano wa jinsi ya kuendesha kesi hiyo.
Jaji Aboud amepangiwa kusikiliza kesi hiyo baada
ya juhudi za usuluhishi zilizofanywa na Jaji Augustine Shangwa
kushindikana, kutokana na Askofu Kakobe kukataa usuluhishi huo.
Katika mkutano huo wa makubaliano ya kuendesha kesi hiyo, kila upande ulitaja idadi ya mashahidi wake.
Katika mkutano huo wa makubaliano ya kuendesha kesi hiyo, kila upande ulitaja idadi ya mashahidi wake.
Upande wa walalamikaji unaowakilishwa na Wakili
Barnabas Luguwa, ulidai utakuwa na mashahidi watano licha ya
walalamikaji wenyewe.
Upande wa utetezi unaowakilishwa na Wakili Miriam Majamba, ulidai utakuwa na mashahidi wanane, zaidi ya mlalamikiwa mwenyewe.
Kesi hiyo namba 79/2011 ilifunguliwa Mei 26, mwaka
jana na wachungaji watatu wa kanisa hilo; Deuzidelius Patrick, Angelo
Mutasingwa na Benedict Kaduma.
Hata hivyo, baadaye Mchungaji Kaduma alilazimika
kujitoa kutokana na ushauri wa ndugu na daktari, baada ya kupata ajali
na kulazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa.
Baadaye, msimamizi wa kanisa hilo wilayani Liwale, mkoani Lindi, Mchungaji Ignas Innocent naye aliwasilisha maombi kutaka kujiunga katika kesi hiyo.
Baadaye, msimamizi wa kanisa hilo wilayani Liwale, mkoani Lindi, Mchungaji Ignas Innocent naye aliwasilisha maombi kutaka kujiunga katika kesi hiyo.
huku akidai ameamua kupigania haki na kwamba, kuna mambo ambayo anataka kuyaweka wazi.
Wachungaji hao wanamtuhumu Askofu Kakobe licha ya
mambo mengine, kwa ubadhirifu wa mali na fedha zaidi ya Sh14bilioni na
ukiukwaji wa katiba ya kanisa hilo.
Awali, Askofu Kakobe kupitia kwa wakili wake,
Miriam Majamba aliwawekea pingamizi la awali walalamikaji hao akidai
hawana haki ya kumfungulia kesi, lakini juhudi zake ziligonga mwamba
baada ya mahakama kulitupilia mbali.
Katika pingamizi lake hilo, licha ya kudai
walalamikaji hawana haki ya kisheria kumfungulia kesi, kwamba si
wachungaji wa kanisa hilo kwani walishafukuzwa tangu mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment