Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa
Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya
Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au
Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier
akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga
wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa
na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye
hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
Kamanda amesema hakuna kona
kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo
Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali
salama kwa sababu haitembei.
Kwenye gari alikua mwenyewe
TAARIFA KAMILI YA KIFO CHA SHARO MILIONEA HII HAPA
No comments:
Post a Comment