INAAMINIKA kuwa mazishi ya Mchekeshaji na mwanamuziki, Hussein Ramadhan Mkiety ‘Sharo Milionea’ hayajawahi kutokea mkoani Tanga.
Mzee
Rajabu (mwenye kofia pichani juu) ni mmoja wa watu wanaomini hivyo,
anasema tangu azaliwe hadi kufikia utu uzima alionao, hajawahi
kushuhudia mazishi makubwa namna ile.
“Nashukru
nimeishi miaka mingi na nimetembea sehemu kadhaa za nchi hii, lakini
sijawahi kuhudhuria msiba wenye watu wengi kama waliojitokeza kuja
kumzika kijana wetu”
“
Amezikwa na watu wengi sana tena wa kila aina inaonyesha kuwa ni mtu
aliyeishi na watu vizuri alikuwa ni kijana mwema sana aliyependa
wenzake,”anasema Babu huyo mkazi wa Lusanga, wilayani Muheza.
Sharo
amepumzishwa jana kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya
familia yao kijijini Jibandeni, Lusanga. Umati mkubwa ulihudhuria
mazishi yake na inakadiriwa zaidi ya nusu ya waliohudhuria, walitoka Dar
es Salaam.
Kitu
pekee ambacho unaweza kujifunza kwenye msiba huu ni kwamba WASANII ni
watu wakubwa sana, labda hawajijui tu, ni watu wakubwa na mashuhuri
pengine kuliko hata wanasiasa wakubwa.
CHANZO-SALUTI5
No comments:
Post a Comment