MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula amekunjua makucha na
kusema walioshinda katika chaguzi za chama hicho kwa rushwa wajiandae
kung’olewa ndani ya miezi sita ijayo.
Mangula alisema hayo jana katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja, jijini Dar es Salaam mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais
Jakaya Kikwete katika sherehe zilizoandaliwa na mkoa wa Dar es Salaam
kuwapongeza kwa kuchaguliwa kwao.
“Wote walioleta malalamiko yanayohusu rushwa
katika uchaguzi watulie, tunayashughulikia, kama kuna mtu alipita kwa
rushwa afahamu kuwa amepoteza,” alisema Mangula ambaye anasema kabla ya
kuteuliwa alikuwa anajishughulisha na kilimo cha nyanya na maparachichi.
Kauli hiyo nzito ya Mang’ula imekuja siku chache
tangu kumalizika kwa chaguzi za ndani za CCM ambazo zililalamikiwa na
baadhi ya makada kwamba baadhi ya walioshinda walitumia kiasi kikubwa
cha fedha kununua kura.
Miongoni mwa chaguzi zilizolalamikiwa ni katika
baadhi ya wilaya na mikoa, lakini zaidi zile za jumuiya za chama hicho;
Umoja wa Wanawake (UWT), Umoja wa Vijana (UVCCM) na Jumuiya ya Wazazi.
Itakumbukwa kuwa ni kutokana na hali hiyo, Rais
alisema waziwazi wakati akifunga mikutano ya UWTna Wazazi na wakati wa
kufungua ule wa UVCCM kwamba vitendo hivyo vitakipeleka chama hicho
kubaya ikiwa havitakomeshwa.
Habari kutoka ndani ya CCM zinasema tayari chama
hicho kimepokea malalamiko mengi kuhusu kukiukwa kwa taratibu za
uchaguzi ndani ya chama hicho nyingi zikihusu rushwa lakini zaidi
zinaztokana na chaguzi za jumuiya za chama hicho.
Mkakati wa Mangula
Jana Mangula alisema atatumia nafasi yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Maadili aliyopewa kuwang’oa waliopata uongozi kwa rushwa na kwamba “hatamwogopa kigogo yoyote wala hatamwonea mtu”.
Mkakati wa Mangula
Jana Mangula alisema atatumia nafasi yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Maadili aliyopewa kuwang’oa waliopata uongozi kwa rushwa na kwamba “hatamwogopa kigogo yoyote wala hatamwonea mtu”.
Alisema watafanya uchunguzi wa kina kwa
waliohusika na rushwa katika uchaguzi huo bila kuihusisha Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
“Hakuna mla rushwa atakayepona katika hili kwa
sababu tunataka kurudisha heshima ya chama chetu ambayo imepotea kwa
sababu ya walarushwa wachache,” alisema Mangula.
Aliongeza kuwa katika uchanguzi huo, hata
waliokuwa wakisaidia kufanikisha rushwa hizo katika uchaguzi huo
watachukuliwa hatua watakazostahili.
Mangula alisema anataka kuwaonyesha Watanzania kwamba hata wakulima wa nyanya wanaweza kufanya kazi ya kupambana na rushwa.
“Namshukuru Kikwete kwa imani yake aliyoionyesha
kwangu hadi akaniteua kugombea nafasi hii, sitamwangusha, nitamwonyesha
kuwa hata wakulima wa nyanya wanaweza,” alisema Mangula huku
akishangiliwa na halaiki ya wana CCM waliofurika kwenye viwanja hivyo.
No comments:
Post a Comment