Zombe na wenzake waliachiwa huru Agosti 17, 2009
na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, dhidi ya ya makosa ya mauaji ya
kukusudia yaliyokuwa yakiwakabili.
Watuhumiwa hao wanarejea tena mahakamani, ikiwa
imepita miaka 3 na miezi 3 tangu hukumu hiyo ya kuwaachia huru
ilipotolewa na aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu wakati huo, Salum Massati.
Hivi sasa Massati ni Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Habari ambazo gazeti hili limezipata kutoka
Mahakama ya Rufaa na kuthibitishwa na baadhi ya maofisa ndani ya
mahakama hiyo zinasema rufaa hiyo itaanza kusikilizwa mwezi ujao.
Mwananchi limefanikiwa kuiona ratiba ya vikao vya
Mahakama ya Rufani ambayo inaonyesha kuwa rufaa dhidi ya Zombe na
wenzake itaanza kusikilizwa tarehe 11Desemba mwaka huu saa 3:00 asubuhi
na Majaji William Mandia, Nathalia Kimaro na Katherine Oriyo.
Watuhumiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka
ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka
Mahenge mkoani Morogoro na dereva wa teksi wa Manzese jijini Dar es
Salaam.
Siku chache baada ya kuachiwa huru, Mkurugenzi wa
Mashtaka (DPP) alikata rufaa Mahakama ya Rufani, akipinga hukumu ya
Mahakama Kuu, akidai kuwa Jaji Salum Massati aliyesikiliza kesi hiyuo
alikosea kuwaachia huru washtakiwa hao.
Katika hukumu yake, Jaji Massati alisema kuwa
upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa
hapo bila kuacha mashaka.
Pia Jaji Massati alisema kuwa amebaini kuwa wauaji
halisi hawajafikishwa mahakamani na kwamba kutokana na kutokuwepo kwao
mahakami, mashtaka dhidi ya washtakwa waliokuwapo mahakamani hayawezi
kutengenezeka, hivyo akaiagiza Jamhuri kuwasaka na kuwafikisha
mahakamani wauaji halisi.
Hoja za DPP
DPP katika rufaa yake namba 254/2009, iliyofunguliwa Oktoba 6, 2009, amebainisha sababu 11 ambazo zimemfanya apinge hukumu hiyo, akidai kwamba kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani, washtakiwa wote walikuwa na hatia.
Hoja za DPP
DPP katika rufaa yake namba 254/2009, iliyofunguliwa Oktoba 6, 2009, amebainisha sababu 11 ambazo zimemfanya apinge hukumu hiyo, akidai kwamba kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani, washtakiwa wote walikuwa na hatia.
Katika hoja hizo, DPP amedokeza kile anachokiita upungufu katika hukumu hiyo, kwa kila mshtakiwa.
DPP anadai kuwa jaji Massati alipotoka, alishindwa
kutafsiri sheria na kanuni mbalimbali zinazohusu mashtaka ya jinai na
kwamba alijichanganya sana katika hukumu hiyo.
Anadai na kueleza kushangaa Jaji kushindwa kuwatia
hatia washtakiwa wote licha ya kwamba kulikuwa na ushahidi wa dhahiri
na wa kimazingira wa kutosha kuwatia hatiani.
No comments:
Post a Comment