MAJRANI
wa familia ya marehemu Sharo Milionea kijijini Jibandeni, Lusanga,
wanasema hawajawahi kuona mtu aliyekuwa anampenda mama yake kama Hussein
(Sharo Milionea).
Mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Saidi
akiwa na kundi la majirani wenzake, aliiambia Saluti5 kijijini hapo
kwamba haujawahi kupita mwezi mmoja bila Sharo kuja kumtembelea mama
yake.
“Alijua
vilivyo majukumu yake, alijua kuwa yeye ndio mhimili wa familia yao,
alihakikisha kila mwezi lazima aje mara moja au zaidi kumsalimia mama
yeke” alisema mzee huyo na kuongeza kuwa msanii huyo alikuwa mtu wa watu
kijijini hapo “Hakulewa sifa, aliendelea kuwa Hussein yule yule
tuliyemlea hapa”.
Inaaminika
Sharo Milionea alikuwa na mipango ya kumfungulia duka mama yake ili
kujikimu kwa shida ndogo ndogo na inasemekena hata miongoni mwa vitu
vilivyoibiwa kwenye gari lake ikiwa ni pamoja na pesa milioni sita
kulikuwepo pia bidhaa kibao mahususi kwa ajili ya duka alililotaka kumfungulia mama yake.
Mama yake ambaye ana ulemavu wa mguu inaaminika atakuwa amepata pigo kubwa sana kwa vile Sharo alikuwa ndio kichwa cha familia.
Kwa
kulewa hilo, Msanii mkongwe, Mzee Majuto aliiambia Saluti5 kuwa
atapambana kadri awezavyo kuhakikisha kuwa mama huyo anapata matunda ya
kazi za mwanae.
Sharo
alifariki kwa ajali ya gari akiwa njiani kwenda kumsalimia mama yake
ambapo alitaka akae nae kwa usiku mmoja kisha kesho yake arejee Dar kwa
ajili ya mazishi ya msanii mwenzake John Stephano Maganga.
No comments:
Post a Comment