
                             Wanajeshi wa Marekani
Maafisa wa serikali ya Japan, 
wamesema kuwa wamewasilisha rasmi malalamiko yao, kwa balozi wa 
Marekani, Mjini Tokyo, baada ya mwanajeshi mmoja wa Marekani kutuhumiwa 
kumjeruhi kijana mmoja raia wa nchi hiyo.
Ripoti zinasema, mwanajeshi huyo aliiingia 
katika chumba kimoja katika kisiwa cha Okinawa, ambako alimpiga mvulana 
mmoja mwenye umri wa miaka 13.Mvulana huyo alianguka kutoka dirishani na alikimbizwa hospitalini.
Uhalifu unaohusishwa na wanajeshi wa Marekani, katika kisiwa hicho cha Okinawa, umekuwa chanzo cha mzozo wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.
Wanajeshi wote wa Marekani nchini Japan sasa wamepigwa marufu, ya kutembea nyakati za usiku, kufuatia tuhuma za ubakaji katika kisiwa hicho wiki mbili zilizopi.

No comments:
Post a Comment