Hatua hiyo ya
Mnyika imekuja baada ya wizara ya Nishati na Madini kutoa matangazo kwenye
magezeti kuhusu rasimu ya sera ya gesi asilia ikiwa katika lugha ya Kiingereza.
“Napinga hatua ya
wizara kutoa rasimu ya sera hiyo kwa kiingereza pekee, natoa wito kwa Waziri
Muhongo atoe kauli kwa umma kuwa rasimu hiyo itatolewa haraka kwa lugha ya
Kiswahili na kuchapwa katika vyombo vingine vya habari,” alisema Mnyika ambaye
ni Waziri Kivuli wa wizara ya Nishati na Madini.
Alhamisi iliyopita,
uliibuka mjadala mkali Bungeni wakati wa kupitishwa kwa azimio la kuridhia itifaki ya uanzishaji wa
kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo Tanzania
ilihimizwa kutumia lugha ya Kiswahili katika taarifa zake kwa wananchi zikiwemo
sera na sheria.
Mnyika alisema
zikichapwa kwa Kiswahili wananchi wengi mijini na vijijini watapata fursa ya
kutoa maoni kwa sababu wataelewa kilichoandikwa kwa kuwa ni wananchi wengi
wanaofahamu lugha ya Kiingereza.
Alisema tafsiri
hiyo ifanyike haraka kwa sababu muda
uliotolewa kwa ajili ya kukusanya maoni na mapendekezo unamalizika
Novemba 22 mwaka huu.
Mnyika pia Profesa
Muhongo kutoa kwa umma ripoti ya awali ya upitiaji upya wa mikataba 26 ya
utafutaji wa gesi asilia ili udhaifu uliojitokeza utumiwe na wananchi katika
utoaji wa maoni katika kuboresha sera ya gesi.
Pia Mnyika alitaka
wizara hiyo kueleza kwanini dola 20.1 milioni zilizopunjwa na kampuni ya Pan
African Energy Tanzania (PAT) hazijarejeshwa Serikalini.
No comments:
Post a Comment