Saturday, November 3, 2012

MAISHA PLUS;Fid Q ndani ya Kijiji leo,Babu aongoza cross country

BABU juzi alionesha kuwa yupo ‘fiti’ kimazoezi baada ya kuwakimbiza ‘cross country’ washiriki katika mapori ya Kijiji, ambako wengi wao walionekana ulimi nje huku wakitamani zoezi limalizike mapema.
Baada ya mchakamchaka huo ulioongozwa na Babu, washiriki walifikia uwanjani, ambako Babu aliendelea kuwapigisha mazoezi ya aina yake, kabla ya kuendelea na shughuli za kijijini.
Wanawake wamsaka ‘mchawi’
Juzi, washiriki wa kike walichukua fursa kuwajadili wenzao waliotoa siri ya kikao chao cha kupendekeza wanaume tishio kutajwa kuingia kikaangoni, ili kutoa fursa ya ushindi kwenda kwa wanawake safari hii.
Washiriki hao Tatu, Debora na Hidaya walikuwa wakijadili hilo, huku wakimlalamikia mmoja wao kujutia suala hilo alipobanwa na wanaume wakati wa kikao chao usiku. Lakini Debora alionekana kubanwa zaidi, kwa kauli yake kuwa alipelekwa pelekwa kuhudhuria kikao hicho cha siri.
Nani kuaga Kijiji cha Maisha Plus leo?
HALI ya wasiwasi inatarajiwa kugubika kijijini leo, kwa washiriki watatu walio kikaangoni.
Washiriki hao ni pamoja na Berenik Kimiro ‘Mama Kevi’, Abdullah Ganiko wa Dar es Salaam na Debora Mwakabenga kutoka Mbeya.
Kati ya washiriki hao, wawili watakiaga Kijiji cha Maisha Plus.
Fid Q ndani ya Kijiji leo
MWANAMUZIKI nyota wa hip hop nchini, Farid Kubanda ‘Fid Q’, leo anatarajiwa kuzuru ndani ya Kijiji cha Maisha Plus na kubadilishana mawazo na washiriki wa kijiji hicho.
Mmoja wa majaji wa shindano la Maisha Plus, Kaka Bonda, alisema kuwa, Fid Q, atapata nafasi pia ya kushuhudia washiriki watakaoaga shindano hilo.

No comments:

Post a Comment