Wednesday, November 7, 2012

Yaliyojiri MAISHA PLUS: Wanakijiji wakutana na uongozi mpya

WANAKIJIJI wa Maisha Plus juzi walikutana na uongozi mpya waliouchagua baada ya wale wa zamani muda wao kuisha.
Uongozi huo chini ya mwenyekiti wake Jonathan…., ulitoa malengo yake na baadaye wanakijiji walipokea ugeni kutoka Benki ya Makabwela ya NMB na kuwapa wanakijiji maelekezo kuhusu huduma na kazi zinazofanywa na NMB.
Kutokana na ufafanuzi wa kina kutoka kwa maofisa wa NMB baadhi ya wanakijiji wametamani kujiunga na benki hiyo.
Pamoja na hayo yote, kazi za uzalishaji mali zinaendelea kijiji hapo ambapo wanakijiji wanazidi kubuni bidhaa mbalimbali.
Aidha Babu amesisitiza kwa wanakijiji kujituma zaidi kwani Jumapili wanakijiji waliuza vitu vyenye thamani ya sh 82,000 mbele ya waheshimiwa wabunge.
Berenik kikaangoni tena
MSHIRIKI Berenik Kimaro kutoka Dar es Salaam, anazidi kuingia katika misukosuko baada ya wanakijiji wenzake kumchagua na kumsababisha aingie tena kwenye hatari ya kutoka.
Benerik ambaye Jumapili alinusurika kutoka, hivi karibuni aliitisha kikao na wanakijiji wa kike na kuendesha kampeni ya kuwatoa wanaume tishio.
Mbali Berenik Kimiro (Dar es Salaam) MP19, wengine ni Justin Bayo (Morogoro) MP 24, Saumu Shaaban (Dar es Salaam) MP10 na Magreth Msechu (Mbeya) MP11, ambapo huruma yao ni kura kwa kuwapigia kwenda namba 15584.
Jonathan azichapa na Kisura
MWENYEKITI mpya Kijiji cha Maisha Plus, Jonathan Joachim, kutoka Singida na mwanakijiji mwenzake Bahati Kisura kutoka Dar es Salaam waliingia kwenye bifu zito baada ya kuchezeana rafu kwenye timu ya mpira.
Washiriki hao, walianza kuzichapa lakini hata hivyo waliyamaliza.
Katika mchezo huo, timu ya Hakuna Stori ilishinda 4 na timu ya Kitimutimu ilishinda 3. Pamoja na hayo yote kutokea Maisha bado yanaendeela ndani ya kijiji.

No comments:

Post a Comment