Meneja wa klabu ya soka ya
Arsenal ya Uingereza, Arsene Wenger, amemsifu sana Theo Walcott, kwa
kuichezea vizuri sana timu hiyo usiku wa Jumanne, katika mechi ambayo
timu hiyo ilitoka sare ya 2-2 katika mechi ya ugenini dhidi ya Schalke
ya Ujerumani.
Walcott, ambaye mashauri ya kuongezewa mkataba
yalivunjika mwezi Agosti, alianza vyema katika mechi hiyo, kwa kuifungia
Arsenal bao la kwanza, na ikiwa ni mara ya nne msimu huu anapoingia
katika mechi tangu mwanzo. Lakini ilikuwa ni mara ya kwanza kucheza tangu mwanzo katika mechi ya Ulaya tangu mwezi Machi.
"Alicheza vizuri sana," alisema Wenger. "Alikuwa ni kati ya wachezaji wetu waliocheza vizuri sana."
Kulikuwa na wasiwasi kama Walcott angelicheza katika mechi ya jana, baada ya kuugua kwa muda, lakini kwa kutokuwepo Aaron Ramsey, ilibidia aingie uwanjani.
Lakini mechi ikielekea kumalizika, katika muda wa majeraha, Walcott alikosa nafasi nzuri ya kuiwezesha Arsenal kuzoa pointi zote tatu.
Kabla ya mechi hiyo, mara zote 12 ambazo ameshirikishwa katika mechi, mara tisa aliingia kama mchezaji wa zamu.
Hata hivyo hayo hayakumzuia kuandikisha magoli saba.
No comments:
Post a Comment