Friday, November 2, 2012

SOMA RIPOTI YA KUHUSU HALI ILIVYOKUA LEO KARIAKOO KTK MAANDAMANO.

Mwandishi wa habari Azizi kutoka Kariakoo ameripoti kwamba makundi ya wananchi ambao wapo Kariakoo yameanza kuondoka Kariakoo kuelekea majumbani kwa sababu hali sio nzuri, polisi wametanda kwenye barabara zote ambapo magari yanayotoka sehemu mbalimbali kuingia mjini yamezuiwa kuingia kutokana na kikundi cha waandamanaji kilichojiandaa kuandamana kuelekea kwenye ofisi ya Waziri mkuu kutawanyishwa kwa mabomu ya machozi na kikundi kikasambaratika.
Polisi bado wanaendelea kudumisha ulinzi ambapo kwa sasa  maduka yamefungwa na mengine yanaendelea kufungwa, shughuli nyingine za kawaida zimesimama na kwa sasa msururu wa watu unarudi kuelekea majumbani, vikundi vya maandamano vimeripotiwa kujikusanya kwenye maeneo tofauti tofauti.
Polisi wanatumia Farasi, Mbwa na magari kusimamia amani ambapo vikundi vilivyojaribu kuandamana vilikua na bendera na wengine walikua na fimbo kabisa, na walikua na gari maalum ambalo walikua wamepanga ndio walitumie kwenda mjini kwenye ofisi ya waziri mkuu lakini polisi wakawawahi na kuwasambaratisha.

No comments:

Post a Comment