Thursday, November 1, 2012

Abiria wasiovaa helment(kofia ngumu) kutozwa faini ya sh30,000 na kufikishwa mahakamani-Morogoro

KIKOSI cha Usalama Barabarani mkoani Morogoro, kimeanza kuwatoza faini ya Sh30,000 na kuwafikisha mahakamani abiria wa pikipiki wanaokiuka sheria ya kutovaa kofia ngumu (helment).
Hatua hiyo inafuatia kupuuzwa kwa sheria hiyo, jambo linalosababisha watu kupoteza maisha.
Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa kikosi hicho mkoani humo, Leonard Gyindo, alipokuwa  akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa madereva 60 wa pikipiki.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la kusaidia WajasiRiamali (APEC) kwa kushirikina na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa  lengo la kufundisha sheria za usalama barabarani na namna madereva hao watakavyoweza kuondokana na umaskini kupitia ujasiriamali.
Katika mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa maofisa wa polisi, Mkuu huyo wa usalama barabarani, alisema uchunguzi wa  polisi umebaini kuwa agizo la kuvaa kofia ngumu kwa abiria limeanza kupuuzwa na kwamba madereva wa pikipiki wamekuwa wakilalamika kuwa abiria wanakataa kuvaa kofia hizo kwa madai kuwa wanaogopa kuambukizwa magonjwa ya ngozi kama mba na fangasi.
Gyindo alisema kufuatia hali hiyo, kikosi kimeamua kufanya operesheni ya kuwakamata abiria wanaoopuuza amri hiyo na kuwatoza faini au uwafikisha mahakamani tofauti na ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wakiwapa adhabu hizo madereva.
“Akikamatwa abiria hakuvaa kofia ngumu atatozwa faini ya Sh 30,000 au kufikishwa mahakamani na kama dereva naye hakuvaa kofia atapewa adhabu hizo kwa mujibu wa sheria na pia pikipiki itafikishwa kituoni kwa ajili ya ukaguzi, ikiwa ni pamoja na bima, leseni na vitu vingine ambavyo ni muhimu katika uendeshaji wa pikipiki,” alisema Gyindo.
Kwa upande wao, madereva wa pikipiki wamekipongeza kikosi hicho, kwa kuamua kuwatoza faini abiria wanaokaidi kuvaa kofia ngumu kwa sababu abiria wenyewe ndio wanaokataa kuvaa kofia hizo kwa madai kuwa wanaogopa kuambukizwa magonjwa ya ngozi.
Mmoja wa madereva hao, Musa Rajabu alisema wao wametii agizo la polisi na Serikali ya mkoa kwa kununua kofia hizo za abiria kwa gharama kubwa, lakini baadhi ya abiria wamekuwa wakikataa kuvaa kofia hizo.
Katika hatua nyingine, Gyindo alisema hivi karibuni kikosi hicho kitaanza operesheni ya kukagua magari ya kubeba abiria yakiwemo mabasi ya mikoani, ili kuupusha ajali zinazoweza kutokea katika kipindi hiki cha kumaliza mwaka.
Alisema kuwa katika operesheni hiyo wataweka vituo mbalimbali vya ukaguzi wa mabasi na kwamba vituo hivyo vitakuwa vikibadilishwa mara kwa mara ili kufanikisha kuwakamata madereva wenye makosa

No comments:

Post a Comment