Sunday, November 4, 2012

Papa mpya wa Copt achaguliwa Misri

Kanisa la Copt la Misri limemchagua papa mpya atayewaongoza Wakristo wanaokisiwa kuwa milioni-8 nchini Misri.
Askofu Tawadros aliyechaguliwa kuwa papa mpya
Papa mpya ni Askofu Tawadros mwenye umri wa miaka 60, na alikuwa msaidizi wa Papa Shenouda wa tatu ambaye alifariki mwezi wa March baada ya kuongoza kanisa hilo kwa miaka 40.
Jina la Askofu Tawadros liliteuliwa na mtoto kati ya majina matatu yaliyoandikwa kwenye vikaratasi vilivowekwa kwenye jagi.
Uteuzi huo ulitokea katika ibada maalumu iliyofanywa katika Kanisa la Saint Mark's mjini Cairo.
Mwandishi wa BBC mjini Misri anasema papa mpya ni mtu mwenye uzoefu mkubwa na maarifa ya uongozi; na kwamba atahitaji sifa hizo katika nchi ambayo inajadili mchango wa Uislamu baada ya mapinduzi yaliyomtoa madarakani Rais Hosni Mubarak.
Msemaji wa chama cha Muslim Brotherhood, kinachoongoza serikali, alinena kuwa wana matumaini kwamba watakuwa na ushirikiano na papa mpya.

No comments:

Post a Comment