Sunday, November 11, 2012

Kutoka kijiji cha MAISHA PLUS: Justin aokota bangi

HALI ni tete kwa Justin Bayo wa Morogoro na uenda akafukuzwa kijijini humo endapo itabainika kuwa mzigo wa dawa za kulevya aina ya bangi alizoziokota ndani ya Kijiji cha Maisha Plus hicho zinamuhusu.
Justin baada ya kuokota mfuko huo wa bangi, aliukabidhi kwa Mwenyekiti wa Kijiji, Jonathan, na yeye kumkabidhi Babu ambaye naye alimkabidhi kaka wa kijiji, Masoud Kipanya.
Mpaka sasa Babu bado haimuingii akilini juu ya nani mwenye mzigo huo wa bangi, huku akisema kuwa, aliyekutwa na ngozi ndie mla nyama.
Justin aliokota bangi hizo kwenye eneo la kukalia wageni mbalimbali wanapofika kijijini hapo.
Hata hivyo, licha ya Justin kuwa kwenye wakati mgumu, Jonathan naye yupo kwenye hatihati kwa tukio hilo kufuatia kutowashirikisha viongozi wenzake na alichoamua Babu ni kuita uongozi wote wa kijiji hicho wakiwemo Gabriel (Makamu Mwenyekiti) na Dola (Katibu) ili kuchunguza zaidi juu ya tukio hilo na kuamua kuwa wafanye msako kijiji kizima.
Uongozi wa kijiji kwa kushirikiana na Babu waliweza kufanya msako mkali ndani ya kijiji hicho, lakini hata hivyo upekuzi huo uliambulia kukuta mipira ya kike aina ya Lady Pepeta (Kondom) na koti.
Kwa mujibu wa Babu, huenda vitu hivyo vilisahaulika na washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula waliokaa kijijini hapo siku za awali kabla ya kuondoka.
Washiriki tumbo joto
WANAKIJIJI Bereniki Kimiro, Justin Bayo, Magreth Msechu na Swaumu Shaban ambao wapo kikaangoni wiki hii, wawili kati yao usiku wa leo watakwenda kukaa kwa siku moja ndani ya Hoteli ya City Style na ‘kula maisha’.
Hata hivyo, mpaka sasa washiriki hao hawajui kitu juu ya tukio hilo na wote wapo kwenye hofu.

No comments:

Post a Comment