Sunday, November 4, 2012

Jumuiya Ya Uamsho na Mihadhara Ya Kiislamu Zanzibar ·

TUNAKUPONGEZA KWA KUSEMA UKWELI...............
UJASIRI WAKO TUNATAKA UWENDELEZE.......
KWAHERI ZANZIBAR...................KARIBU TANZANIA..           .


Napenda kuchukua fursa hii kuweza kumpongeza kwa dhati Makamo wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Katibu Mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sherif.
Kiukweli sitaki kusema wala kurejea nyuma nini aliongea jana natumai wazanzibar wote wanayo habari nini aliongea jana katika viwanja vya Kibata Maiti.
Ila ukweli aliousema ndio kitu ambacho muda mrefu wazanzibar walikuwa wanakisubiri kwa hamu kwani toka awe madarakani miaka 2 sasa ameshindwa kufurukuta na kushindwa kuzungumza ukweli kwa kuikemea serikali yake hadharani inapofanya makosa.

Jana aliweza kuwabakisha na kuwafanya watu wawe midomo wazi washindwe kuamini kweli huyu ndie maalim Makamo wa kwanza wa Rais au ni Katibu Mkuu wachama maneno kama yale alikuwa akiongea kuanzia mwaka 1995,2000,kwa kweli tumefurahi natunampongeza kwa kuzungumza ukweli na kuwa mjasiri na kuweza kuwapa matumaini wazanzibar.
Labda niweke wazi sina lengo la kuichukia serikali hii ya umoja wa kitaaifa kiukweli nilifahamu kuwa serikali hii ni ya cuf na Karume ndio wanayoitaka hao wengine ni kubabaisha watu tu,ndio mana tulikuwa tunamkanya Maalim kuwa alikuwa anaanza kupelekwa pabaya na serikali yake bila yeye kujitambua ila tunashkuru kujua kuwa hawa ccm hawana nia yadhati ya ukombozi wa nchi hii.
Ila sasa naanza kupata mashaka kama serikali hii itafika kweli 2015?
Jee ushirikiano upo kwa Mawaziri?
Vipi Baraza la Wakilishi litaendelea kama zamani kuibana serikali na kushirikiana?
huu mpasuko ulikuwepo ndani ya seikali ya GNU nahisi kama sasa wizara za cuf ndio cuf na ccm ndio ccm.
Wallahi ninamaswali mengi ambayo nafikiria na kosa majibu.
Nasema tena mimi sio mfuasi wa chama chochote ila niko hapa kwa kuongea ukweli,akifanya makosa tutamzungumza pia akisema ukweli tutampongeza na hiyo ndio sifa ya Uislamu.
Sasa naanza kupata wasiwasi kuhusu hii tume ya Katiba ambayo wazanzibar wengi walikuwa wanaambiwa tume tume kila kitu kaseme katika tume sasa nawauliza wana cuf na ccm Uamsho tulivosema hatutaki muungano tumeambiwa tunakosea tusubiri tume tukatoe maoni tusiisusie maneno mengi yalizuka.
sasa hiyo tume maalim haiyamini tena lakini uamsho walivosema hawakuaminiwa wakaonekanwa wanataka kuvunja masalahi ya vyama sasa mimi nauliza MKOMBOZI WA ZANZIBAR NI NANI IKIWA TUME PIA HAIFAI...?

Mwisho kwa kumalizia na omba nimzungumze Shein ambae Rais wenu na Makamo wenu Seif Idd,tusipowaangalia hawa kwa macho mawili mimi naona msimamo wangu zanzibar itatutoka.
Shein na Makamo wake hawana uchungu hata kidogo na zanzibar wako hapo kwa maslahi yao na Kwamslahi ya Watanganyika tu ndoomana leo wanalani kuchomwa kwa MABAA,KUVUNJIWA MABIA NA MASKANI ZAO ZAKISHENZI lakini hawalaani Raia wanavopigwa na kudhalilishwa na Jeshi lao ndio Kwanza anawapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kupiga watu KWELI MTU HUYU BADO MUNAIMANI NAE.?
Mimi kama mimi ambae muuno wangu mdogo na sina elimu ya kutosha ila navofahamu kidogo katika Dini hakuna makubaliano na madhwalimu tunao mfano tosha wa mtume wetu Muhammad s,a,w alipotaka kufunga mkataba wahudaibia masharti waliyaweka yote yana masalahi na wao na pia waliuvunja mkataba wenyewe.
Cha msingi tusidanganye kushirikiana nao hawa kuwa nao pamoja katika serikali tutapata afuweni mfano tosha munao uchaguzi wa BUBUBU,Nachokusudia kusema maadhi ya kizidi kila moja achukue mbao zake huwezi kushirikiana na dhwalimu halafu ukategemea utapata faida hilo haliwezekani abadani.

Wazanzibar tuamke zanzibar haiwezi kupatikana kwa kukaa katika meza kufanya mazungumzo naapa wallah thumwa wallah zanzibar katu haitopatikanwa kwa njia ya KATIBA MPYA wala haitopatikanwa kwa mseto wa cuf na ccm wala haitppatikanwa kwanjia ya kukaa katika meza na watanganyika.ZANZIBAR itapaitikanwa tukiwa wa moja tukawa wakweli tukajenga ushirikiano tukadai zanzibar yetu kwa njia ya People Power bila ya kujali vifo vitakavotokea hilo ni lazima kama nchi inatakiwa kweli.
Lau kama kweli unapenda pepo basi huwezi kuogopa kifo.
Ila kama tutaendelea kukaa kwenye barza ya kahawa na kupeana drip za uongo na kweli basi tuendelee na uoga huo.

KWAHERI ZANZIBAR.......... KWAHERI UISLAMU.
KARIBU TANZANIA.................KARIBU UKAFIRI.

No comments:

Post a Comment