Mshindi wa mwaka jana, Yaya Toure, anaongoza
katika orodha hiyo yenye majina ya wachezaji 10, waliochaguliwa kutoka
orodha ndefu ya wachezaji 34. Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast,
ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Manchester City, ni kati ya
wachezaji wanne wanaozichezea timu za Uingereza ambao huenda wakapata
tuzo hiyo ya mwaka 2012. Kiungo cha kati wa Chelsea, John Obi
Mikel, mshambulizi wa Arsenal, Gervinho, Demba Ba wa timu ya Newcastle,
ni kati ya wachezaji wengine wa ligi kuu ya Premier ambao wanawania tuzo
hiyo. Katika orodha hiyo, kuna wachezaji wengine ambao waliwahi kucheza Uingereza mwaka 2012.
Wachezaji
hao ni aliyekuwa kiungo cha kati wa Arsenal, Alexandre Song, na ambaye
sasa huichezea Barcelona ya Uhispania, na mshambulizi wa zamani wa
Chelsea, Didier Drogba, ambaye anaichezea klabu ya China, Shanghai
Shenhua. Chris Katongo ni mchezaji wa pekee kutoka timu ya Zambia iliyoibuka mshindi katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Mchezaji
wa Morocco, Younes Belhanda, yumo katika orodha hiyo, kwa juhudi zake
mapema mwaka huu, katika timu ya Ufaransa ya daraja ya kwanza,
Montpellier.
Wanaowania tuzo hiyo, watapunguzwa hadi kufikia watatu, katika wiki ya mwisho ya mwezi Novemba.
CAF
vilevile ilitangaza orodha fupi ya wachezaji watano, ambao wana nafasi
ya kupata tuzo la mchezaji bora barani Afrika, kwa wachezaji ambao
hucheza kandanda yao barani Afrika.
Katika ordha hiyo ni pamoja
na Mohamed Aboutrika, kiungo cha kati kutoka Misri, na aliyecheza katika
mechi ya Al Ahly ya klabu bingwa dhidi ya Esperance ya Tunisia, mchezo
uliokwishwa kwa sare ya 1-1 siku ya Jumapili.
Tuzo hizo, ambazo
zitakuwa pia ni kumpa zawadi kocha bora zaidi wa mwaka, na klabu bora
zaidi mwaka 2012, zitatolewa kwa washindi tarehe 20 mwezi Desemba,
katika ukumbi wa Banquet, katika ikulu ya rais, katika mji mkuu wa
Ghana, Accra.
No comments:
Post a Comment