Waziri mmoja wa Sri Lanka
amekataa wito wa waziri mkuu wa Uingereza kwamba ufanywe uchunguzi wa
kimataifa kuhusu madai ya uhalifu wa kivita uliofanywa mwisho wa vita
vya wenyewe kwa wenyewe vya nchi hiyo.
Waziri wa maendeleo ya kiuchumi, Basil
Rajapakse, ndugu wa Rais Mahinda Rajapakse, aliwaambia waandishi wa
habari kwamba uchunguzi kama huo kamwe hautoruhusiwa.Matamshi yake yanafuatia tamko la waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, kwamba Uingereza itauomba Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi wa kimataifa, iwapo Sri Lanka yenyewe haikuanzisha uchunguzi utaojitegemea ufikapo mwezi wa March.
Bwana Cameron alisema hayo nchini Sri Lanka ambako anahudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za Jumuia ya Madola.
Ijumaa Bwana Cameron alikutana na Rais Mahinda Rajapakse.
No comments:
Post a Comment