Tuesday, November 19, 2013

Huyu ndo muuaji aliyeua watu watatu kwa bastola jijini Dar leo.....Kisa na mkasa ni wivu wa mapenzi


Mapema leo asubuhi milio ya risasi zaidi ya kumi ilisikika eneo la Ilala Bungoni karibu na baa maarufu ya Wazee (Club ya Wazee), watu watatu wakiripotiwa kufariki kutokana na tukio hilo linaloelezwa kuwa limetokana na wivu wa kimapenzi.
 
Dereva mmoja wa tax kituo cha Bungoni ambaye alikuwa shuhuda wa kwanza, alisema mapema leo asubuhi alipata mteja aliyehitaji kupelekwa sehemu, ila kabla hawajafika huko walipokuwa wanataka kwenda jamaa ambaye ndiye alikuwa ni muuwaji alimuomba akatishe safari na kumtaka ampeleke sehemu nyingine.
 
Dereva  huyo  aliendelea kusimulia  kuwa  alimpeleka jamaa mpaka aneo la tukio hilo kwenye nyumba iliyopo pembeni mwa Hotel mpya iitwayo MM.
 
Mara baada ya kufika hapo, jamaa alitoa sh. 5,000 na kumkabidhi dereva ila cha kushangaza ni kitendo cha jamaa huyo kutoa bastola wakati akiwa anaelekea kwenye geti la nyumba.
 
Wakati jamaa anaelekea getini mlango ulifunguliwa na gari aina ya Toyota Surf ilitoka ikiwa na watu wanne ndani, mwanaume mmoja ambaye alikuwa akiendesha gari , mama mmoja na wadada wawili.
 
Jamaa akiwa na bastola alianza kuwashambulia watu waliokuwa ndani ya gari hilo na kumpiga risasi dereva na mdada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Carol...Baada  ya  dreva  tax  kuona  hali  imechafuka  ilimbidi  akimbie.
 
Vyanzo vingine vinaeleza kuwa katika tukio hilo jamaa pia alimpiga risasi ya mgongoni mama wa mwanamke aliyemuua na pia alimpiga msichana mwingine risasi ya mguu.
 
Mtuhumiwa na dereva aliyekuwa akiendesha gari walifariki palepale huku msichana mmoja akielezwa kufariki akiwa njiani kuelekea hospitali.
 
Bado haijafahamika moja kwa moja chanzo cha mauaji hayo licha ya watu wengi kudai  kuwa  ni  wivu  wa  mapenz

No comments:

Post a Comment