30/11/2013
Nikiwa
kama Mtanzania ambaye kwa sehemu moja au nyingine nawajibika katika
utumishi wa jamii, nimeona vema nitoe mawazo yangu kidogo kuhusu
kinachoendelea ndani ya CHADEMA kama taasisi. Mimi sio mwanasiasa kwa
maana ya kimajukumu wala kiutendaji lakini ni sehemu ya siasa za nchi
yetu kwa cheo changu cha Uraia wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wengi wetu tunafahamu au tumesikia sintofahamu inayoendelea katika CHADEMA kama taasisi. Pamoja na ukweli kuwa huenda sisi ambao tuko nje ya taasisi hii hatujui kwa undani yanayoendelea ndani ya chama hicho, lakini kwa sehemu kubwa wahusika wa taasisi hii wamekua wakitoa habari nyingi tunazokutana nazo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na kwa jinsi hiyo picha ya kinachoendelea iko wazi kwa sehemu kubwa.
Kwa mfuatiliaji yeyote wa mambo ya siasa na uongozi katika nchi yetu anaelewa vema uendeshwaji wa taasisi za kisasa katika nchi yetu. Kwa wiki kadhaa sasa nimekua nikifuatilia kwa karibu habari na mijadala iliyokua ikiendelea pamoja na kauli mbalimbali za wanachama, viongozi na wabunge wa chama wa CHADEMA. Kwa mtazamo wangu kuna mambo

kadhaa
yanakanganya na mengine yako wazi kabisa kwa maana ya chanzo cha
mgogoro. Mambo mengi yamekua wazi zaidi hasa baada ya waraka wa
kimkakati katika kuleta mabadiliko katika uongozi wa chama hicho kuwekwa
hadharani na kufuatiwa na yaliyojiri katika mkutano wa kamati kuu na
muendelezo wake.
Nianze kwa kusema kuwa, migogoro ni afya katika kundi na jamii yoyote ile. Migogoro ni chachu ya fikra chanya na pana katika kuibua tofauti zenye kujenga na kuondoa nadharia ya amani iliyolala katika kundi na taasisi. Migogoro ni afya kubwa kwa sababu inapotokea ndio unakua wakati muafaka wa kutuwezesha kufahamiana kwa undani kuwa sisi ni watu wa aina gani; nini kimehifadhiwa ndani ya mioyo na dhamira zetu; na kwa nini tunafanya na kutenda mambo fulanifulani. Migogoro huondoa wingu linalozuia kutabaniasha taswira halisi ya ndani kati utu wa mwanadamu usio kamili.
Migogoro inakua tatizo tu katika mazingira makubwa matatu:
Mimi sio mwanachama wa taasisi hii wala sijawahi kukutana uso kwa uso na wanaoshutumiwa wala kuwa na mawasiliano nao kama viongozi. Nimewafahamu kwa kazi yao na uwajibikaji wao katika taasisi yao na kama vile ambavyo inawezekana kuna wengi wanakubali mchango wao katika kuijenga taasisi, hata mimi nimeshawishika na mchango wao katika mambo ya msingi ndani na nje ya taasisi yao. Hivyo maoni yangu hayajajikita katika kuwatetea bali katika ukweli uliofungwa na nadharia ya ubinadamu unaokuba kuwa kutokamilika kwetu sio msingi wa utambulisho wetu. Pamoja na hili, iwapo kuna mambo ya msingi wale wanaoshutumiwa wameharibu, ni wajibu wao kujitazama na kukubali fikra mpya zinazolenga kuwasaidia kuwa watu bora zaidi.
Huenda wanapata vita zaidi kutokana na ugumu wao katika kukubali fikra na misimamo tofauti na waliyonayo au kujitambulisha kuwa bora zaidi ya wengine hasa pale kunapotokea mambo ya msingi yenye kuhitaji mustakabali wa pamoja.
Mwalim MM
mathewmndeme@gmail.com

- Moja
ni pale tunapouangalia zaidi wasifu wa muhusika katika mgogoro
(personality) na kuushambulia utu wake na hivyo kujikuta tunapambana
naye zaidi badala ya chanzo na mgogoro wenyewe.
- Pili
ni pale tunapotatua migogoro kwa matukio badala kwa kuangalia chanzo
cha mgogoro. Hili limekua tatizo kubwa sana katika nchi yetu. Mara
nyingi tunahangaika zaidi na mtukukio na kuacha kujikita katika msingi
wa matukio huku tukiwa tumedharau ukweli kuwa huwezi kuelezea utatu na
uchachu wa chungwa bila kuhusisha na mti wake pamoja na ulivyotunzwa
kabla na wakati wa kubeba machungwa husika.
- Tatu, migogoro inakua tatizo pale ambapo wahusika katika mgogoro wanapokosa hekina na ufahamu sahihi wa kushughulikia migogoro.
- Nakiona
chama husika kuwa kwenye wakati mgumu wa kukubali kuiweka nadharia ya
demokrasia kwa ujumla wake katika vitendo. Kama taasisi ambayo bado
inakua huku ikiwa imebeba majukumu kadhaa ya kiuongozi katika taifa,
jambo hili linaweza lisiwe la kushangaza sana lakini inategemewa kuwa
baada ya miaka zaidi ya 20 sasa, lazima kuwa na dhamira njema za
kuongeza wigo wa kidemokrasia katika taasisi.
- Kama
ilivyo kwa vyama vingine vya upinzani, wengi walioingia humo kama
wanachama wameingia kwa malengo binafsi zaidi na ni wachache ambao
wameamua kuwa wanachama wa vyama vya upinzani kwa malengo ya kutafuta
njia mbadala ya kisiasa na kiuongozi katika kulisaidia taifa letu. Ni
changamoto kuwa na taasisi ambayo wengi wa walioko ndani wana malengo
binafsi ya uongozi au kupata fursa ambazo zinapatikana ndani ya chama au
nje kupitia chama
- Kutokana
na hoja 2 za kwanza hapo juu, chama hiki kiko katika wakati mgumu wa
kufanya kazi kama taasisi na badala yake imekua kama vile baadhi ya watu
ndani ya chama ndio wenye nguvu na majina yao kuwa maarufu kuliko
taasisi. Ujasiri huu wa watu hawa ndani ya chama ndio unaokipa chama
wakati mgumu kwani kila mmoja anataka kujiimarisha yeye kama taasisi
badala ya kukijenga chama kama taasisi.
- Tatizo
la tatu hapo juu linakifanya chama kiwe na watu wengi walioko busy na
mikakati ya kujijenga wao binafsi badala ya kujenga taasisi. Ni kweli
kuwa hakuna mtu yeyote asiyekua na mikakati ya kujijenga kama mtu
binafsi lakini ni lazima mikakati hii itanguliwe na mitakati ya
kitaasisi na kijamii maana hivi vikifanikiwa ni rahisi na mtu binafsi
kufanikisha malengo yake. Kinyume chake huwa ni majanga. Ni lazima
tuwaze kufananikiwa kama taifa kwanza kabla ya kuwaza kujifanikisha mtu
mmoja mmoja ...na hili tatizo ni majanga makubwa katika taifa letu.
..Kila mmoja anaanza na mimi kwanza wengine baadaye iwapo kutakua na
kitakachobakia.
- Tatizo
la kimfumo wa kitaasisi ni kubwa na linaonekana zaidi pale ambapo
kwenye chama hicho karibu kila mmoja ni msemaji wa hisia/maamzi/mtizamo
na mipango ya chama. Ukienda kwenye mitandao unaona kabisa jinsi ambavyo
wanachama wenye ushawishi ndani ya chama hicho huwa wepesi sana kutoa
kauli zainazobeba sura ya kitaasisi kama vile wanakisemea chama.
- Kuwa
na wanachama wengi kwenye chama ambao wamejikita katika kutafuta
kujijenga wao binafsi, kumepelekea wanachama hawa (na hata viongozi wao)
kutazamana kwa hisia za kutaka kuzibiana. Na matokeo yake taasisi
imejikuta ina watu amboa wanawindana, wanaharibiana, wanashindana,
wanapambana na hata kuvunjiana heshima latika kutafuta kufanikisha
malengo binafsi.
- Hoja
ya sita inaweza kuthibitishwa na jinsi ambavyo tangu sintofahamu
iliyokikuta chama itokee, unashangazwa na wingi wa wanachama na viongozi
wa chama hicho wanaoonesha chuki ya hali ya juu kwa walioshutumiwa kuwa
ni wakosaji. Inasumbua kweli kuona jinsi ambavyo kukikosea chama (iwapo
kuna kosa) kunabadilika kuwa ni kukosea watu binafsi na hivyo kujenga
hoja ya kuonesha chuki na uadui wa hali ya juu na hata kushindwa
kuheshimiana.
- Taasisi
yoyote imara lazima iwe na mpango mkakati wa muda mrefu wa jinsi ya
kutatua matatizo yanayojitokeza bila kujali ukubwa au udogo wake. Ni
lazima taasisi ijijengee utamaduni wa kutatua migogoro kwa haraka na
kuimaliza bila kuiacha kukua na kubadilika majanga kwa taasisi. CDM wana
changamoto hii.
- Chama
hiki kijiwekee malengo yenye mipango ya kutekelezeka katika kukijenga
kama taasisi. Pamoja na mambo mengine, lazima ibuni njia na miundombinu
ya kiutawala na kujiendesha ili utaasisi wake uwe dhahiri, wa kweli na
wazi kwa jimii
- Lazima
taasisi hii iwe na mkakati wa kudumu wa namna nzuri ya kupata viongozi
wanaoaminishwa siri za chama na uendeshwaji wake. Tatizo la majina na
umaarufu kua na nguvu kuliko taasisi ambalo nimelitaja hapo juu,
limejitokeza sana CDM hasa pale watu maarufu wanapotoka vyama vingine au
huko walipokua na kupewa madara makubwa ambayo ni wazi wanakua hawana
mizizi ya kutosha katika kuyasimamia. Mara nyingine wageni hawa
wanaokaribishwa moja kwa moja hadi jikoni na chumbani, huwa wanakuja na
malengo yao ambayo mara nyingi yanakua sio ya kikimarisha chama
- Chama
hiki kikubali kuiweka ndaharia ya uongozi wa uwajibikaji katika
matendo. Badala ya kutumia nguvu kubwa katika kujibizana, kuzibana
midomo na kujibu hoja zinazoonesha manung’uniko, malalamiko na shutuma;
vionngozi wake watumie nguvu kubwa kufanya mambo ya vitendo huku
wakijitahidi kusikiliza na kufanyia kazi malalamiko ya wale
wanaowangoza.
- Ni
vema kama taasisi ikubali kujitathmini katika kuukubali ukweli hata
kama unauma na haupendezi kwa baadhi ya watu au vingozi. Hii ni njia
pekee itakayoweza kukifanya kielewe nini jamii inachotaka kuingoza
inataka na kutegemea kutoka kwao
- Kuna
msemo usemao, “usianze kutafuta soko la ngozi ya simba kabla hujamuua
kwanza maana mwisho wa siku unaweza kujikuta simba ndio kakuua
wewe”....kwa lugha yao husema, ”Don’t sell a skin before you kill a
lion”. Taasisi hii isishangilie ushindi au kujiona washindi kabla
hawajakabidhiwa ushindi. Ni vema kuwa na subira katika harakati zake
katika kuuendea ushindi iwapo uko dhahiri. Subira hii ina mambo mengi ya
msingi kujijenga zaidi, kujiimarisha zaidi na kujitawala zaidi.
Viongozi wasijenge kiburi cha kukubalika na kujiona wajuaji bila kutaka
kujua nini watu wanategema kwao.
- Wanachama
na viongozi wa taasisi husika waache kuwapa uzito wanachama au viongozi
fulani kuliko chama na badala yake kuwa na usawa wa kuheshimiana katika
ujenzi wa taasisi. Ni hatari sana kumwangalia mtu mmoja au kikundi cha
watu wachache kama msingi wa ukuaji na kusimama kwa taasisi kwani hakuna
mwanadamu mwenye mkataba na Mungu wa kuishi hadi jioni au kesho
asubuhi. Mojawapo wa mikakati wa kulitendea kazi hili ni kuhakikisha
dhana ya uongozi ni ya wazi, ya kubadilishana kwa moyo wa amani, na
yenye uwajibikaji mkubwa kwa wanaoongozwa
- Ni
lazima wahusika wote ndani ya chama wajitahidi sana kuchuja kile
wanachokiongea kwenye umma...bila kujali ni kwenye vyombo vya habari,
mitandao ya kijamii au kwingine popote pale. Hii itawezekana tu pale
ambapo wale ambao ama wamejipa au wamepewa umaarufu na ushujaa katika
chama watajiona umuhim wao ni sawa na wa wengine...na tofauti ziko tu
kwenye utendaji na uwajibikaji tu na sio ubora. Chama kiwe na nidhamu
katika kuyaongelea mambo ya chama kwani ni hatari kuwa na nyumba ambayo
baba, mama, watoto na hata ndugu na wafanyakazi walio ndani wote ni wa
semaji wa familia
- Taasisi
hii ijitahidi kung’oa mzizi wa uadui, majungu na mashindano ndani ya
chama. Badala ya kubomoana, kama kuna anayeonekana ana neema, vipaji na
mtazamo wa kujenga taasisi na nchi kuliko wengine, basi huyu apokee
msaada wa kila aina katika kumfanya kuwa bora zaidi ili hatimaye aweze
kuwa msaada wa kuiinua taasisi na wale wa nje ya taasiso kwa maana ya
nchi yetu.
- Wanachama
wa taasisi hii watenganishe maswala ya kitaasisi na ya kibinafsi.
Hakuna mantiki ya mtu kusemekana kakikosea chama au katiba ya chama
halafu akageuka ni adui wa kushambuliwa, kutukanwa, kudharauliwa na
kutothaminiwa. Haifa kuwa na chama ambacho mama akilaumiwa na chama au
wanachama, mume wake ambaye sio kiongozi wa chama anaibuka na kujibizana
na wahusika. Ni ngumu kuwa na chama ambacho baba akishindwa kuwajibika
kwenye uongozi wake mke wake au watoto wake wanatoka na kukisema chama
au kutoa ufafanuzi. Ni lazima kutenganisha mambo ya familia na taasisi.
- Taasisi
hii na wanachama wake wajitahidi sana kuwa na malengo ya pamoja na
kuyafanyia kazi pamoja. Katika nadharia ya uongozi na menejimenti, umoja
na mshikamano miongoni mwa viongozi ni jambo la muhim sana bila kujali
tofuati za utu wao. Kila kiongozi ndani ya taasisi ni vema ajione ni
sehemu ya taasisi na ajizuie kwa gharama zozote zile kujitambulisha yeye
binafsi nje ya utambulisho wa taasisi yake huku akijua hata kama
anaweza kufanya alifanyalo kwa utambulisho wake,mwisho wa siku
anaiaibisha au kuijengea heshima taasisi yake
- Ni
hatari sana kwa taasisi kudharau mchango wa wanachama na viongozi wake
kwa sababu tu kuna makosa wamefanya. Katika ubinadamu wa kawaida ni
udhaifu mkubwa sana kufuta mema yote ya mtu kwa sababu ya kosa au
kuonesha upande wa pili tusioupenda. Pamoja na majukumu mengine, taasisi
lazima itumike kusaidia wanachama na viongozi wake kuwa bora zaidi na
wanapoonesha kasoro zisizokubalika basi wajikite zaidi katika
kuwarejesha badala ya kuwaona hawajawahi kuwa na faidia na ni hasara kwa
chama
- Mwisho
kabisa, nikishauri chama hiki kuangalia vema namna wanavyokwenda
kutatua sintofahamu iliyoko katikati yao. Wajaribu kutizama kwa undani
uzito wa makosa ambayo yameonekana kwa baadhi ya viongozi wao (kama ni
kweli) ambao nina hakika wamekua sehemu na mchango mkubwa sana wa
kilipofikia chama sasa hivi. Pamoja na makosa yao (kama wanayo),
wakumbukwe pia kwa mema na michango yao na kwamba kuna wakati walisimama
kwa niaba ya chama kwa namna ambayo hakuna mtu mwingine yeyote yule
angefanya. Mara zote, kuridhiana na kukubaliana ni bora zaidi ya
kushutumiana, kulaumiana, kulumbana, kuchafuana na kuhukumiana.
Mimi sio mwanachama wa taasisi hii wala sijawahi kukutana uso kwa uso na wanaoshutumiwa wala kuwa na mawasiliano nao kama viongozi. Nimewafahamu kwa kazi yao na uwajibikaji wao katika taasisi yao na kama vile ambavyo inawezekana kuna wengi wanakubali mchango wao katika kuijenga taasisi, hata mimi nimeshawishika na mchango wao katika mambo ya msingi ndani na nje ya taasisi yao. Hivyo maoni yangu hayajajikita katika kuwatetea bali katika ukweli uliofungwa na nadharia ya ubinadamu unaokuba kuwa kutokamilika kwetu sio msingi wa utambulisho wetu. Pamoja na hili, iwapo kuna mambo ya msingi wale wanaoshutumiwa wameharibu, ni wajibu wao kujitazama na kukubali fikra mpya zinazolenga kuwasaidia kuwa watu bora zaidi.
Huenda wanapata vita zaidi kutokana na ugumu wao katika kukubali fikra na misimamo tofauti na waliyonayo au kujitambulisha kuwa bora zaidi ya wengine hasa pale kunapotokea mambo ya msingi yenye kuhitaji mustakabali wa pamoja.
Mwalim MM
mathewmndeme@gmail.com
Source: http://www.wavuti.com/4/post/2013/11/maoni-ushauri-wa-mwalimu-mm-kwa-wahusika-wa-sintofahamu-ndani-ya-chadema.html#ixzz2m8wagwyy
No comments:
Post a Comment