Moshi. Uongozi wa Kijiji cha
Kiria, Kata ya Mamba Kusini wilayani Moshi, Kilimanjaro umeiomba
Serikali na taasisi zinazojihusisha na ukatili wa kijinsia kumsaidia
mtoto mwenye umri wa miaka 13 aliyebakwa na kulawitiwa na baba yake
mzazi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Doroth Mtui alisema
mtoto huyo kwa sasa amehifadhiwa kwenye nyumba ya msamaria mwema na
anahitaji matunzo na kupelekwa shule, jambo ambalo serikali ya kijiji
imeshindwa.
Mtui alisema mtoto aliyekuwa darasa la kwanza
kabla ya kuachishwa shule, anahitaji kuishi sehemu tofauti na mazingira
ya nyumbani ili kumnusuru na tatizo la kisaikolojia.
Mtui alisema mtoto huyo alipaswa kurudishwa
hospitalini wiki mbili toka alipofanyiwa uchunguzi 0ktoba 9 mwaka huu,
lakini mpaka sasa hajarudishwa kwa vile hakuna mwenye uwezo wa
kumsaidia.
“Uchunguzi unaonyesha kuwa ameharibika vibaya
sehemu za siri na ameota nyama kwa ndani. Alipewa dawa na anatakiwa
kurudi tena kwa ajili ya uchunguzi,” alisema Mtui.
No comments:
Post a Comment