Awali, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa
Chadema hicho, Benson Kigaila alieleza maazimio ya Kamati Kuu ya chama
hicho kuhusu kujipanga kuanzia ngazi ya chini mpaka taifa.
Pia aligusia suala la kugatua madaraka kutoka
makao makuu kwenda katika Kanda 10 pamoja na Progamu ya Vuguvugu la
Mabadiliko (M4C), ambayo utekelezaji wake ulikuwa na awamu nne
unaombatana na mafunzo mbalimbali.
Kuhusu uchaguzi, alisema kuanzia Novemba 22 hadi 14 Desemba,
mwaka huu ni kipindi cha kukamilisha usajili wanachama kuanzia ngazi ya
chini.
“Tarehe 15 Desemba mpaka 15 Januari, 2014
utafanyika uchaguzi katika ngazi za vitongoji. Kuanzia tarehe 16
Januari hadi 30 Januari, 2014 kitakuwa kipindi cha kukata rufaa na
kukagua ukamilifu wa uchaguzi wa ngazi hiyo,” alisema Kigaila na
kuongeza:
“Februari 1 hadi 15 mwaka 2014, utafanyika
uchaguzi ngazi za matawi (vijiji kwa vijijini na mitaa kwa mjini),
kuanzia Februari 16 hadi 29, itakuwa kipindi cha kukata rufaa na ukaguzi
kwa ngazi hiyo.”
Alisema kuwa kuanzia Aprili Mosi hadi 10, 2014
utafanyika uchaguzi ngazi ya majimbo ya uchaguzi ambayo yapo 236 na
kuanzia Aprili 25 mpaka Mei 5, 2014 utafanyika uchaguzi ngazi ya wilaya.
Alisema kuanzia Mei 20 mpaka 25, 2014 utafanyika
uchaguzi ngazi za mkoa na Juni 6 hadi 9, 2014 utafanyika uchaguzi katika
Kanda zote 10 na Juni 23 mpaka 30, 2014 utafanyika uchaguzi ngazi ya
taifa.
No comments:
Post a Comment