CCM kwa chafuka, Kigwangalla awavua nguo Spika Makinda, Filikunjombe na Kangi Lugola
Nimeona hawa nisiwaache wapotoshe umma kwa maslahi yao binafsi, acha niwajibu.
Kwanza, niseme hapa wazi kwamba, ni mwendawazimu tu ama mtu asiyeelewa
mahusiano ya Mhe. Deo Filikunjombe (Mb.) na Mhe. Spika Anne Makinda
(Mb.) ama na Mhe. Kangi Lugora (Mb.), atakayepata tabu kuelewa kwa nini
watu hawa wamenishambulia kwenye magazeti na mitandao ya kijamii. Deo
Filikunjombe ni 'mtoto wa mama' Anne Makinda!
Pili, niseme pia kwamba watu wa aina hii hawakustahili kujibiwa lakini
kwa ushauri wa wabunge wengi wanaoniunga mkono nimeamua niwajibu. Hawa
wabunge wenye kuja na nyoka wa dhahabu bungeni na kujigamba wao ni
majasiri kwa kuwa 'walisaini karatasi ya hoja ya kumng'oa Waziri Mkuu na
baada ya kushughulikiwa na wabunge wenzao wa CCM walianza kulia lia kwa
Mwenyekiti wa Chama kuwa wasamehewe kwa kuwa waliasi chama kwa sababu
wamebanwa sana majimboni mwao na wanaCCM wenzao na pia na wapinzani',
kwa hakika hawakustahili majibu toka kwangu. Tabia za ukinyonga namna
hii ni ujasiri, udandiaji hoja ama kutokujua wanalofanya ndani ya Bunge?
No comments:
Post a Comment