Maoni ya ALBERTO MSANDO(mwanasheria maarufu na diwani wa CHADEMA) -juu ya majibu ya mnyika na lisu
Kinachofanywa na hao wote ni siasa na usitegemeae reasoning yako ya
kisomi au kisheria kwao ina maana yoyote. Wao lengo ni moja
kumshughulikia Zitto.
Mbowe alishapanga toka akiwa Kilimanjaro
kwamba anaenda kumtoa Zitto. Ushahidi ninao. Vikao vya pembeni
vilishafanyika kumtoa Zitto. Ushahidi ninao. Hii ni siasa chafu.
Wanacholalamika kwamba Mwigamba na Kitila wamefanya na wao ndicho wanachokifanya!!
Turudi kwenye msingi wa hoja yangu.
Katiba ya Chadema inasema kiongozi au mwanachama apewe mashtaka yake
kwa maandishi na ajibu kwa maandishi. Ndipo aitwe kwenye kikao ajadiliwe
hatua zichukuliwe.
Hilo ni jambo ambalo taasisi au mfumo wowote wa haki na utawala bora utafuata.
Marekebisho ya Katiba hayakugusa kipengele hicho hata kidogo.
Kilichobadilishwa ni kipengele cha (b) na (c) ambavyo wanatakiwa
wavisome. (Naamini wamevisoma na ndio maana hukusikia hilo likijibiwa
jana).
Pia hata hivyo vipengele vilivyorekebishwa vinasema kuwe
na dharura kwamba 'maslahi' ya chama (sio ya viongozi au Kamati Kuu)
yako hatarini ndio vikiukwe.
Tatizo hapa wengi mnaliangalia hiki suala kwa jicho la woga 'itakuwaje bila Chadema. Au CCM itapeta Chadema wakigombana'.
Mko tayari ku compromise mawazo huru na kukosoa ukiukaji wa misingi ya
utawala wa Sheria na utawala bora kwa ajili tu ya kuitoa CCM madarakani.
Hiyo ni dhambi.
Chadema hakiwezi kudhoofika kisa tu wanachama
au viongozi tunapingana iwe hadharani au kwa siri. Hilo linaweza kutokea
kwenye madhehebu ya dini ukisema Yesu sio Mungu wakati wewe mkatoliki
au Ukamkana mtume SAW wakati wewe muislamu. Kumpinga kiongozi sio uhaini
wala usaliti.
Kupanga mkakati kumshinda kiongozi kwenye
uchaguzi wa kikatiba tena kwa siri sio MAPINDUZI. Sasa mtu alitakiwa
aanze kuandika mkakati wake mwezi mmoja kabla ya uchaguzi? Halafu
atekeleze vipi? Mkakati huo haukuwahi kuwekwa public. Hata walivyoukuta
kwenye computer ya Mwigamba wao ndio waliusambaza. Kwa nini?
Tusione wachache ni Malaika na wengine ni shetani. Wote ni Malaika wote ni Shetani kwenye siasa tunazozishuhudia.
Kuna watu watahusisha urafiki. Ni kweli Zitto ni rafiki yangu.
Wanasahau Mbowe na Mnyika ni marafiki zangu pia. Mbowe ni Msimamizi
wangu wa Ndoa. Akili yako ikuongoze wakati wa kufikiria.
Barua zikipokelewa zitajibiwa. Tuendelee na majadiliano tuache woga na kuficha ficha mambo ya msingi.
Albert. —
No comments:
Post a Comment