Mashindano ya GOtv Cecafa Senior
Challange yatang’oa nanga siku ya Jumanne huku timu 12 zikishiriki
kwenye mashindano hayo yanayo husisha timu kutoka kanda ya za Afrika
Mashariki na Kati.
Makocha wa timu zote wamewaita kambini wachezaji
wao bora wakiwemo wale wanaocheza ugenini ili kuongeza nafasi zao za
kushinda kombe hilo.Hela pia zitatolewa kama zawadi zimepangiwa ambapo kitita cha dola 100,000 zitagawanywa kati ya washindi watatu bora na hii ni baada ya kampuni ya Gotv kutoa udhamini wa dola 125,000 za kimarekani.
Mechi zitachezwa katika miji ya Nairobi, Kisumu, Nairobi na Machakos huku serikali za wilaya zikitoa udhamini na kushawishi kumbi ambapo mechi hiyo itaandaliwa- kwa kurejelea mashindano ya vilabu bingwa ya mwaka huu yalioandaliwa katika miji ya darfur na kusini mwa kordofan nchini sudan.
Mashindano ya cecafa yamesalia kuwa chanzo cha furaha katika soka haswa kwa mashabiki wa eneo la afrika magharibi na kati haswa ikizingatiwa kuwa timu kutoka eneo hili hazijapata nafasi ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa kutokana na viwango duni vya soka nchini.
Ukosefu wa wadhamini umesababisha kubadilishwa kwa jina la mashindano ya mechi za cecafa mara kwa mara kwa heshma za wadhamini.
Tanzania wamewaita washambulizi wa TP mazembe Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata ili kuonyesha uzito wa mashindano ya mwaka huu.
Mashindano ya klabu bingwa yameitwa baada ya rais wa Rwanda Paul Kagame huku Senior Challenge yakipewa jina la bwenyenye wa Ethiopia Sheikh Mohammed al Amoud kati ya 2005 na 2006.
Mashindano ya mwaka huu yatakayoisha tarehe 5 Disemba yanajumuisha timu 11 za kanda na Zambia ambao ni wageni.
Kundi A linajumuisha Kenya, Ethiopia, Sudan kusini na Zanzibar, kundi B ni Tanzania, Zambia, Burundi na Somalia, kundi C linahusisha mabingwa watetezi Uganda, Rwanda, Sudan na Eritrea.
Ni timu 4 pekee zimeweza kufuzu kwa kombe la Afrika katika mda wa miaka 10 huku 1 pekee ikishiriki hatua ya makundi.
Rwanda na Kenya zilifika Tunisia 2004, Sudan ilishiriki fainali Ghana 2008 na 2012 huko Equitorial Guinea huku Ethiopia ikishiriki Afrika Kusini 2013.
Cecafa ilianzishwa mwaka 1926 wakati huo ikijulikana kama Kombe la Gossage wa utawala wa ukoloni Kenya, Uganda,Tanganyika na Zanzibar, lakini mwaka wa 1967 ilibadilishwa jina na kuwa senior challenge cup na imekua ikiandaliwa mara kwa mara lakini imeshindwa kuhamasisha ushindani jambo ambalo limechochea mjadala kulifanya shindano hili kuwa la kuendeleza timu za vijana.
No comments:
Post a Comment