Kwa kutumia mfumo mpya ufaulu wa Kidato cha Nne mwaka jana ungekuwa asilimia 94
Dar es Salaam.Wakati Mtihani wa
Taifa wa Kidato cha Nne nchi nzima ukiendelea, imebainika kuwa madaraja
na alama mpya za ufaulu kwa shule za sekondari zilizotangazwa na
Serikali hivi karibuni ni tofauti na zile zilizopendekezwa na Kamati
Maalumu iliyoundwa kuchunguza suala hilo pamoja na zile zilizotolewa na
makundi mbalimbali yaliyoshiriki kuandaa mfumo huo mpya.
Mbali na kwenda kinyume na maoni hayo, alama hizo
zinaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na viwango vya
chini vya ufaulu.
Alama hizo zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome zinaonyesha
kwamba: A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na
F=0-19, huku alama endelevu za upimaji wa mwanafunzi shuleni (Continuous
Assessment-CA) ikiwa ni 40 na mtihani wa mwisho ukichangia alama 60.
Kabla ya Serikali kutangaza alama hizo mpya,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliunda Kamati Maalumu iliyopewa
jukumu la kufanya uchunguzi na kuja na mapendekezo ya viwango vipya vya
ufaulu na utaratibu wa CA.
Kamati hiyo ilifanya kazi hiyo na kukabidhi ripoti
yake wizarani Septemba mwaka huu na mapendekezo yake kwenye upangaji wa
alama hizo ilikuwa ni A= 80-100, B= 70-79, C= 50-59 D= 40- 49, E= 35-
39 na F= 0-34 huku wakitaka CA iwe alama 25.
Baada ya kuandaliwa kwa ripoti hiyo, Serikali
ilitafuta maoni zaidi kutoka kwa wadau wengine kupitia makundi
mbalimbali ambayo nayo yalitoa mapendekezo.
Kundi la kwanza lililotoa mapendekezo yake ni
Jukwaa la Taasisi za Elimu za Serikali ambalo lilitaka ufaulu uanzie
alama 40, kundi jingine ni Vyuo vya Watu Binafsi ambalo lilipendekeza
ufaulu uanze alama 35 huku Wakuu wa Vyuo vya Serikali na Wakaguzi Wakuu
wa Kanda wakitaka ufaulu uanzie alama 40 na CA iwe 30.
Ofisa mwandamizi kutoka Baraza la Mitihani la
Taifa (Necta), ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema
kitaalamu CA hutakiwa kuwa chini ya alama ambayo inahesabika kuwa ndiyo
ufaulu.
Alisema baada ya Serikali kupitisha mfumo ambao
ufaulu unaanzia 20, ilitarajiwa CA kuwa chini ya 19 badala ya 40
iliyopitishwa na wizara.
Ufaulu wa chini
Kwa mujibu wa kitabu kinachoonyesha viwango vya
ufaulu duniani kila mwaka cha International Qualification, baada ya
Tanzania kutangaza alama hizo mpya, sasa inakuwa nchi inayoongoza
duniani kwa kuwa na alama za chini za ufaulu.
No comments:
Post a Comment