Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limeomba kuongeza
bei ya umeme kwa asilimia 67.87 ikiwa ni kutoka Sh197.8 kwa Unit mpaka
Sh332.06.
Hayo yamebainishwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa
Tanesco, Felchesmi Mramba, alipokuwa akiwasilisha maombi ya shirika hilo
mbele ya Wadau wa Umeme na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji
(Ewura).
Alisema kwa sasa
uzalishaji wa umeme utokanao na nguvu za maji ni asilimia 13, utokanao
na gesi ni asilimia 42 na utokanao na mitambo ya mafuta ni asilimia 45.
“Kutokana na kuongezeka kwa gharama za kutoa huduma, wastani wa bei
iliyopo ya Sh197.8 kwa uniti, hailingani na wastani wa Sh332.06 kwa unit
inayotakiwa kukidhi mahitaji ya sasa,” alisema Mramba na kuongeza:
“Hii ni pungufu kwa kiasi cha Sh134.25 kwa uniti, ongezeko la bei la asilimia 67.87 litafidia upungufu huo,” alisema Mramba.
No comments:
Post a Comment