Actor huyo mahiri ambaye ameigiza katika movie zote za Fast & Furious na movie kali iitwayo Lazaru’s Project, ameripotiwa kufariki dunia jumamosi ya jana ambapo yeye na rafiki yake walikuwa kwenye gari aina ya Porsche iliyokuwa ikiendeshwa na rafiki yake huyo, gari hilo lilikosa muelekeo likiwa katika mwendo kasi na kugonga mti na kisha kulipuka hapo hapo.
Actor huyo na rafiki yake walipata ajiali hiyo kubwa wakitokea kwenye moja ya kampeni yake ya kutoa msaada iitwayo Reach Out Worldwide, kaskazini mwa jiji la California Los Angeles. Habari hizi za kutokea kwa ajali na kifo cha walker pamoja na rafiki yake zimethibitisha kupitia mtandao wa kijamii wa facebook wa actor huyo. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.
No comments:
Post a Comment