Mbunge wa Arusha Godbless Lema aamuwa kugawa picha za Kugushi za kumdhalilisha!!
Mbunge wa Arusha Mjini mh Godbless Lema ameamuwa kugawa picha zilizokuwa
zikisambazwa ktk mitandao ya Kijamii zikimuonyesha akilawitiwa.
Hii imetokea ktk mkutano wa leo unaofanyika ktk viwanja vya Kilombero jijini Arusha.
Picha hizo ni zile za kutengeneza zikimuonyesha mtu mwenye sura inayofanania na yeye.
Katika hali ya kushangaza baada ya Mh Mbunge Lema kumuita Mke wake
(Neema) ili azigawe picha hizo ambazo alikuwa ameziprint kwa wingi,
Wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo walikataa picha hizo kugawanywa na
kusema hazina umuhimu wowote ila zichomwe moto kwa kuwa wanajua ni za
kutengeneza wala hazina ukweli wowote.
Baada ya ubishani ndipo mh Mbunge aliamuru kura zipigwe na waliosema picha zisigawanywe walishinda.
Ndipo picha zikachomwa moto na Mh mbunge kuwashukuru wapiga kura wake
kwa kuonyesha heshima kwake kwa kukataa picha hizo kugawanywa ktk
mkutano huo. Mkutano unaendekea........!
No comments:
Post a Comment