Mkutano wa wakristo waliopoteza makao yao kufuatia ghasia Nigeria
Kundi la kiisilamu la Boko Haram
nchini Nigeria, na vikosi vya usalama, wote wametuhumiwa na shirika la
kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International kwa kufanya
vitendo vya kukiuka haki za binadamu hasa katika eneo la Kaskazini lenye
waisilamu wengi.
Boko Haram, ambalo jina lake linamaanisha elimu
ya kimagharibi imeharamishwa, kufanya harakati za kuiangusha serikali na
kuunda taifa la kiisilamu.Ingawa hawajakiri kufanya mashambulizi hayo, kundi hilo limewajibika wakati lilipofanya mashambulizi Kaskazini na kati kati mwa Nigeria.
Obadiah Diji, kiongozi mmoja wa vijana wa kikristo mjini Kaduna, alisimulia BBC ambavyo maisha yamebadilika mjini humo.
“ watu wanaogopa hata kutoka nje usiku au hata kukaa nje tu kunywa pombe au hata kula samaki.
Nimeishi mjini Kaduna karibu maisha yangu yote na nimejawa na huzuni sana nikiona ambavyo umegawanyika sana kwa ,misingi ya kidini.
Waisilamu wanaishi ambako idadi yao ni kubwa, wakristo nao vile vile. Kwa hivyo makundi hayo mawili ya watu, yanaishi maisha yao kivyao bila kutangamana
Sio kawaida kuwa hivi. Wakati mmoja tulijivunia kwa sababu ya umoja uliokuwa unadhihirika hapa Kaduna na kila mtu alikuwa anakaribishwa hapa.
No comments:
Post a Comment