SIKU chache baada ya Makamu Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) Taifa, Philip Mangula, kujibu mapigo ya wapinzani wake akisema
wanaombeza wanasahau historia yake, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk.
Willibrod Slaa, amemtaka aweke mikakati hiyo katika vitendo.
Dk. Slaa alidai kuwa kwa sasa Watanzania wamechoka kusikiliza
historia, hivyo kama Mangula ana uthubutu aanze kusafisha chama chake
kwa kuwaondoa watuhumiwa magwiji wa ufisadi kabla ya kuhangaika na wale
waliotoa rushwa kwenye uchaguzi wao.
Wakati Dk. Slaa akitoa somo hilo kwa Mangula, naye mwanasiasa mkongwe
nchini, Thomas Nyimbo, amemvaa kigogo huyo wa CCM akisema kuwa ni kama
anashindana na kivuli chake kwa kujidanganya kuwa ataitokomeza rushwa
ndani ya chama hicho.
Kauli hizo zinakuja siku chache baada ya Mangula kakaririwa na vyombo
vya habari akitamba kuwa wanaombeza kuwa hawezi kuitokomeza rushwa CCM
wanasahau rekodi yake akiwa Katibu Mkuu wa chama hicho.
Mangula bila kumung’unya maneno aliwataja wafanyabiashara Yusuf Manji
na Thomas Nyimbo kuwa ni miongoni mwa watu aliowafutia ushindi
wasigombee ubunge baada ya kubainika kujihusisha na rushwa katika kura
za maoni mwaka 2000.
Mwanasiasa huyo pia alikumbushia jinsi chama kilivyofuta matokeo ya
baadhi ya washindi katika majibo 32 na kuamuru uchaguzi urudiwe baada ya
kubaini uwepo wa mizengwe ya rushwa, hivyo akaahidi kuwa wanaombeza
wangoje waone ndani ya miezi sita atakavyochukua hatua.
Hata hivyo, katika mahojiano yake na gazeti hili jana, Dk. Slaa
aliendelea kumbeza Mangula akisema kama anajisifu kuwa anaweza kuondoa
wala rushwa katika CCM, basi aanze na watuhimiwa sugu walioshindikana
kung’oka kwenye falsafa ya kujivua gamba.
Alisisitiza kuwa anamshangaa Mangula kwa kujisifu kwa jambo hilo, na
kwamba kama kweli anaweza basi atekeleze sera ya kujivua magamba
iliyomshinda mtangulizi wake Pius Msekwa na Wilson Mukama.
Alisema kuwa watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho ambao
wametajwa hadi na wana-CCM wenyewe bado wapo na wanaendelea vema na kazi
za kila siku.
“Hivyo kama Mangula ana ubavu aanze na hawa aache kujisifia historia,
mambo anayoyataja kwanza Watanzania wengi hawayajui, wanataka kuona
sasa,” alisema.
Baraza la umoja wa mataifa limepitisha kwa kauli moja kwa wingi wa kura kupandisha hadhi ya eneo la Palestina.
Nchi mia moja thelathini na nane ziliunga mkono
hatua ya kuitambua Palestina kuwa nchi ambayo si mwanachama wa Umoja wa
mataifa lakini itaruhusiwa kushiriki katika shughuli za umoja wa
mataifa.Mataifa tisa yakijumuisha Isarael na Marekani yalipiga kura ya kupinga mpango huo huku mataifa arobaini na moja yakisusia shughuli hiyo.
Kura hiyo yenye umuhimu mkubwa sasa inaiwezesha Palestina kuwa na ushirika na umoja wa mataifa na mashirika mengine kama vile mahakama ya ICC.
Mwandishi wa BBC amesema kuwa wapelestina wanaweza kutumia nafasi hayo kuishataki Israel kwa kusababisha visa vya dhulma dhidi ya ubinadamu katika ngome yake.