Tuesday, December 31, 2013

RASIMU YA 2 YAKATIBA TOA MAONI JINA NA MAHALI



Raisi Jakaya Kikwete amevisihi vyama vya siasa nchini kuweka kando tofauti zao ili kupata katiba bora kwa manufaa ya watanzania wote.

Rais alikuwa akikabidhiwa rasmi rasimu ya pili ya katiba huku mapendekezo mengi ya wananchi yakipendekeza uwepo wa muundo wa serikali tatu.

Ni katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo Makabidhiano hayo yamefanyika mbele ya Raisi wa Jakaya Kikwete na rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein hatua inayoashiria kuanza kwa uundaji wa bunge maalumu la katiba.

Rais Kikwete Amesema kazi ya tume tayari imekwisha kilichobaki sasa ni kwa wajumbe ambao watakaobahatika kuingia katika bunge la katiba wasitangulize maslahi yao bionafsi kwani kazi wanayoenda kuifanya huko ni kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.


Kwaupande wake raisi wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema tangu kuanza kwa mchakato huo serikali yake imeanza kuzitambua changamoto mbalimbali kutokana na maoni yaliyotolewa na kuanza kuyafanyia kazi.

Amesema hatua hiyo iliyofikia inaipa heshima kubwa Taifa hivyo amewataka wajumbe ambao watateuliwa kuingia katika uwakilishi wa bunge la katiba wajue kuwa wanawajibu mkubwa kutumia nafasi hiyo kwa busara kwa niaba ya wananchi.



Joseph Warioba ni Mwenyekiti wa tume hiyo amesema pamoja mambo mbalimbali kujitokeza katika tathimini ya tume hiyo sula kubwa lililojitokeza ni muundo wa serikali tatu.

Hapa ni baadhi ya wanasiasa waliohudhuria hafla hiyo
Mkabidhiano hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.

No comments:

Post a Comment