Hapana shaka wapenzi wa soka
barani Afrika pamoja na kuomboleza kifo cha Nelson Mandela wamekuwa
wanafuatilia Droo ya kombe la dunia kufahamu nani wapinzani wa timu tano
zinazowakilisha bara hilo.
Cameroon wamejikuta katika kundi gumu la A pamoja na wenyeji Brazil, Mexico na Croatia.Dua ya Ivory Coast ya kuepuka kundi gumu sana wakati huu inaonekana imesikika, wako katika kundi C pamoja na Colomboa, Japan na Ugiriki.England watakuwa na kibarua kigumu kwenye kundi D ambapo wapinzani wao ni Italia, Uruguay na Costa Rica.
Kwenye kundi E Ufaransa inacheka usiku huu kwani imepangwa pamoja na Uswizi, Ecuador na Honduras.Mabingwa wa Afrika Nigeria wako katika kundi F pamoja na Argentina Iran na Bosnia Harcegovinia, ambayo inashiriki kombe la dunia mara ya kwanza.
Ghana ndiyo inayoonekana kuwa matatizoni miongoni mwa timu za Afrika. Wamejikuta katika kundi G ambapo watapamaba na na Ujerumani, Marekani na Ureno.Timu ya tano ya Afrika Algeria itakuwa kwenye kundi H na wapinzani hapo ni Ubelgji, Korea Kusini na Urusi.
No comments:
Post a Comment