Friday, December 27, 2013

Marekani:uchaguzi ufanyike haraka A.kati


Marekani imesema kuwa inasikitishwa na machafuko yanayoendelea nchini Jamuhuri ya afrika ya kati, huku Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akizitaka mamlaka kufanya uchaguzi haraka iwezekanavyo.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry
Watu kadhaa wameuawa wakiwemo walinda amani kutoka nchini Chad kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati maafisa nchini humo wameeleza.
Walinda amani hao walishambuliwa na kundi la wapiganaji wa kikristu wanaofahamika kwa jina la anti-balaka shambulio lililotokea mjini Bangui siku ya jumatano.
Shirika la misaada la msalaba mwekundu limesema Watu wengine takriban 40 wameuawa tangu siku ya jumatano.
Vikosi vya Umoja wa Afrika na vya Ufaransa vinafanya jitihada za kukomesha mgogoro kati ya makundi ya kikristo na kiislamu yaliyopamba moto nchini humo.
Umoja wa Afrika umepeleka wanajeshi wake 4,000 nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati. Ufaransa ambalo ni koloni la zamani la nchi hiyo likiwa na Wanajeshi wake 1,600 kwa ajili ya kuimarisha hali ya usalama.
Wanajeshi wa Ufaransa wakiwa kwenye doria mjini Bangui
Wanamgambo kutoka jamii ya kikristo na kiislamu wamekuwa wakishambuliana tangu Mitchel Djotodia alipokuwa Kiongozi wa Taifa hilo baada ya kumuondoa madarakani Francois Bozize anayetoka jamii ya kikristo.
Wakristo wengi wamekuwa wakiishutumu Serikali ya Chad kuwa na uhusiano na Waasi wa Seleka waliomuweka madarakani Djotodia, huku waislamu nao wakishutumu majeshi ya ufaransa kuwa yamekuwa yakishirikiana na wanamgambo wa kikristo

No comments:

Post a Comment