Friday, December 27, 2013

Tulipokonywa ushindi asema Rodgers



Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers, ameshutumu wasimamizi wa mechi yao na Manchester City, ambayo walishindwa kwa magoli mawili kwa moja.
Rodgers ametaja utendaji wa marefa wa mechi hiyo kua ya kusikitisha sana.
Brendan Rodgers
Kocha huyo aligadhabishwa na uamuzi wa msaidizi wa refa wa kuinua bendera kuashiria kuwa Rahim Sterling alikuwa ameotea na hivyo kuwanyima bao halali.
Pia kocha huyo anasema walinyimwa penalti pale Luis Suarez alipoangusha ndani ya eneo la hatari.
Rodgers amehoji ni kwa nini kocha huyo kutoka Bolton alichaguliwa kusimamia mechi hiyo.
'' Nilishangazwa sana kuwa tunacheza katika uwanja wa nyumbani wa Manchester, na refa kutoka eneo hili kuteuliwa kusimamia mechi yetu'' Alisema Rodgers.
Ameongeza kusema kuwa ni matarajio yao kuwa siku zijazo hawatamteua refa kutoka eneo hilo kusimamia mechi yao na Manchester City.
Kabla ya mechi hiyo Liverpool ilikuwa ikiongoza ligi kuu ya premier, lakini kufuatia matokeo hayo, sasa imeshuka hadi nafasi ya nne na alama tatu nyuma ya vinara wa ligi hiyo kwa sasa Arsenal, ambao waliishinda West Ham kwa magoli mawili kwa moja.

No comments:

Post a Comment