Thursday, December 26, 2013
Mwanamuziki wa Injili Kutoka Afrika Ya Kusini Pastor Solly Mahlangu-Aomba URAIA WA TANZANIA
Mwanamuziki wa Injili Kutoka Afrika Ya Kusini Pastor Solly Mahlangu amewataka Wanamuziki wa Injili Tanzania Kuwa "Washirika" katika Makanisa yao na Pia Kutumika Chini ya Wachungaji Wao. Mwanamuziki Huyo ambaye siku ya Jana ndiye aliyepagawisha Uwanja wa Taifa aliwaeleza kuwa kabla ya Kupata Mpenyo katika Albam yake ya 3 yenye jina la Obrigado alikuwa akitumika chini ya Pastor wake kwa miaka 27 ndipo Bwana akampa Mpenyo wa Kutumika Kimataifa.
Mbali na hapo mwanamuziki huyo alieleza kuwa anakusudia kutuma maombi kwa Serikali ya Tanzania kupitia Mgeni rasmi Mhe. Lukuvi kuomba uraia wa Tanzania na ikimpendeza Mungu Moja ya Albam zake kuja ku-shoot Live katika ardhi ya Tanzania ambako anahisi ana biological and divine connection. Mwanamuziki huyo alieleza kuwa ambavyo mmoja wa kaka zake Solomon Mahlangu inasadikika alizikwa hapa Tanzania katika Mkoa wa Morogoro eneo la Mazimbu na ndio maana nyimbo zake katika Albam lazima Wimbo wa Kiswahili uwepo. Alienda mbali zaidi alipoeleza kati ya watoto wake watatu watoto wake wawili amewapa majina ya Kiswahili. Hivyo basi anaamini kabisa ana Utanzania mwingi ndani yake....gonga hapa twende zetu.....http://samsasali.blogspot.com/2013/12/mwanamuziki-solly-mahlangu-anakusudia.html
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment